MBWEMBWE ZA FUNDI 06


 


"Karibu James! Hapa ndio nyumbani kwetu"

"Ahsante sana Madam Scola" Akaitikia huku akiweka miwani yake vizuri. Wakaongozana hadi juu ya ghorofa, akakutana na Mwanamke anayeitwa Jolie ambaye ndiye Anayetarajiwa kuolewa na Balozi, Uzuri wa Jolie ulimfanya Fundi James asahau kwa muda tukio lililotokea ndani ya Gari, akasahahu kabisa kama ana mkasa kuhusu ile kamera iliyo mrekodi akiweka vizuri Mashine yake.


Hakika Familia hii ilikuwa na Wanawake warembo sana.

"James huyu ndiye anayetakiwa kushonewa nguo anaitwa Jolie!!"

"Oooh! Karibu sana James" Kwakuwa James alisema waende haraka awahi kurudi kazini, kazi ya kumpima Jolie ikaanza.

Ndani ya Moyo wa Fundi James akajisemea kuwa tangia ameanza kazi ya kushonea watu nguo hakuwahi kukutana na Wanawake warembo na wenye pesa kama Jolie na Scola, maumbo yao yalikuwa makubwa yenye ushawishi wa hali ya juu sana.


Kila alipokuwa akipitisha kipimo kwenye mwili wa Jolie alijikuta akisisimka sana hasa ukizingatia Fundi James alikuwa Lijali

"Nipo nje!" Akaongea Scola na kuwaacha Jolie na Fundi James wakiwa wanendelea na vipimo.


Jolie alikuwa ndani ya Khanga moja tu licha ya kumuona James lakini hakushtuka kabisa, akafanikiwa vipimo kwa sehemu kubwa akabakisha eneo la kiuno ambalo lilikuwa linampa wakati mgumu sana James. Akajikuta akijikoholesha mara kwa mara, pale ndani Palikuwa pamewashwa feni ya chini hivyo kuna wakati Khanga ya Jolie ilikuwa ikipeperuka na kufanya sehemu ya paja lake liwe wazi, akapeleka kipimo ili apate saizi ya kiuno.


Kiuno kilikuwa laini sana, James alifanikiwa kuligunduwa hilo baada ya kuzungusha kipimo na kukibana pembezoni mwa kiuno cha Jolie. Kwa jinsi alivyokibana ilimfanya Jolie ajisikie vibaya, yaani kama alifanya makusudi vile wakati anapeleka kipimo akabinya kidogo kiuno

Comments