MBWEMBWE ZA FUNDI 05


 


"Sio vibaya! Nimeolewa"

"Oooh! Hongera sana"

"Asante!! Oh My God hili gali huwa silipendi kabisa yaani muda wote kamera inaturekodi tuu, hebu bonyeza hapo pembeni" akamuonesha mahali, James akabonyeza ili kuzima


"Ina maana ilikuwa inarekodi tokea tunaanza safari?" Akauliza kwa mshangao

"Ndio, yaani hadi uzime...ukiwasha gari nayo inawaka na kurekodi kwa ajili ya usalama...ni gari ya mdogo wangu ambaye anaolewa" Sura ya James ikawa ndogo kama piritoni aliposikia kamera ilikuwa ikirekodi kila kitu pale ndani ya gari, ina maana kama ilikuwa ikirekodi basi hata James alipoitoa mashine yake na kuirudisha kwenye Chupi alikuwa amerokodiwa. Akatamani amwambie Scola wafute kilichorekodiwa lakini akahofia kuulizwa sababu ya kufanya hivyo ni nini na asingeliweza kumwambia kuwa alikuwa ametoa mashine ndani ya gari.

"Mbona kama una mawazo James? Hauko sawa ingawa sikufahamu sawa sawa lakini unaonekana hauko sawa kabisa" Akauliza Scola huku akimtazama James.

Bado James alikuwa kwenye mshangao wa hali ya juu, safari iliendelea wakati Scola akiwa amekosa jibu kamili la Fundi James juu ya hali yake jinsi ilivyo Badilika ghafla.


Scola aliendelea kukanyaga mafuta kuitafuta Mikocheni, ilipata mishale ya saa 6 Mchana jua likiwa linawaka vilivyo. Paja lake halikumsisua tena James kutokana na mawazo lukuki yaliyokuwa yamekitawala kichwa chake, James akafungua maji aliyonunuliwa kisha akanywa kidogo ili kutuliza mawazo aliyonayo.


Baada ya masaa mawili walikuwa wameshafika mikocheni na sasa gari lilikuwa linasimama kwenye maegesho ya magari kwenye nyumba hii ya kifahari, nje akapata kuona magari mengine ya kifahari yakiwa kwenye maegesho.

Comments