Sehemu ya 2
Nilishangaa sana mzazi anawezaje kumkana mtoto na kumpa mtu hata asiemjua siku zote nilikua najua baba hanipendi lakini nilikua najipa moyo ila kupitia haya nilijihakikishia kweli sipendwi nililia sana moyoni sikupenda aunt lola aone machozi yangu. tulianza safari na aunt lola maana tulitumia gari yake aliyokuja nayo akiwa na dereva wake tulitembea sana tukaja kulala njiani sikujua ni wapi kwani nilikua mgeni sana ila aunt lola alinichukulia chumba nikaambiwa nioge kisha nae alienda chumbn kwake sikuona dereva alipoelekea ila baada ya muda aunt alikuja chumbn kwangu akiwa amevaa pensi fupi akasema anatoka mimi nitulie chumbn nitaletewa chakula humo nikasema sawa akatoka mmh nilimtafakari jamani mbona kikaptula kifupi ivo na top ile ipo wazi sana sehemu kubwa ya nyonyo ilikua wazi mmh nikajua mambo ya kizungu haya aunt lola alionekana mtu mwenye pesa zake bwana nilitulia chumbn nikaletewa chakula chips na kuku na juisi kubwa ya box nilifurahia mnoo nikala na kunywa juisi kidogo mana niliogopa kunywa nyingi nisije ota ndoto za kukojoa nikalowesha godoro kubwa la watu nilimaliza nikaanza angalia tv mana waliniwashia nashangaa kabisa kwetu hakunaga hizo ilikua niliangalia miziki hadi nikapitiwa na usingizi nilikuja amshwa kumekucha naambiwa nioge tukanywe chai tuendeleea na sfari nilifanya ivo kisha safari ikaendelea dereva aliendesha mpaka mwanza tulifika usiku kama mid aya saa tatu ivi nilisinzia nikastuka naamshwa naambiwa shuka tumefika basi nilishuka kuna dada mmoja alikua anasaidia kubeba mizigo tukaiingiza ndani mmh nyumba ni nzuri ina sofa kwetu kulikua na mbao hata kwa mzee temba pia mbao lkn hapa mmh tv kubwa ukutani redio na spika ndefu kimeza cha kioo nilishangaa aunt lola akasema manka karibu hapa ndio kwa aunt yako lola. Nikasema asante aunt akaita suziii Yule dada aliitika akaja akasema mpeleke manka kwenye chumba nilichokuambia huyu ni mtoto wa kaka angu ivo mimi ni aunt yake naomba mlee hivo suzy akasema sawa dada, aunt lola akasema huyu ni dada etu hapa nyumbn muheshimu sawa nikasema sawa. Basi nilipelekwa chumbn sikuamini mie naenda lala kwenye chumba hiko ni kizuri sana kina kitanda kikubwa madirisha makubwa na kabati ukutani pia kuna bafu na choo ndani dada suz alikua ananionesha, nilipewa mashuka na blanket nikaambiwa nioge kisha nitoke tukale. Nikasema sawa basi niliingia bafuni nikaoga sikuwa na nguo za kubadili mana sikua na nguo kabisa zaidi ya mbili alizonipa mtoto wa mzee temba.nilioga nikavaa zile zile nikatoka aunt nae alikua kuoga akaja na dereva nae akaingia kutokea nje niliitwa sehemu ya kulia chakula nikakaa na aunt lola na dereva tukala msosi wa maana kisha nikaambiwa nikapumzike nilienda kulala lakini kama kawaida usingizi ulikata mapema ivo niliamka nikakuta dada suzy ashaamka nikamsaidia kazi japo alinikataza nikasema hapana asijali nilifanya kazi kwa bidii hadi dada suzy akanipenda.aunt aliamka akakuta tushapika chai akasema manka nawe uliamka saa ngapi?nikamwambia mapema akasema sio lazima suzy ndio anatakiwa awahi mana analipwa kwa ajili hio sawa nikakaa kimya mana sikukubaliana na hilo aunt aliaga anaenda kazini akasema manka nitarudi mchana jiandae nikupeleke ukanunue nguo mana hueleweki kabisa nikasema sawa aunt asante basi alitoka mimi nilibaki na tv sasa maana hakukua na kazi mchana nilisaidian ana dada suzy kupika kisha tukala aunt akampigia suzy simu akasema aniambie kuna boda inanifata niende nikasema sawa basi bodaboda alifika nikajiandaa nikaenda nikamkuta aunt huko mjini mimi nilikua nashangaa jinsi mji wa mwanza ulivo nilikua mshamba mno, nilinunuliwa nguo nzuri na aunt akaninunulia na masuruali nikashindwa kukataa maana nilikua sipendelei nguo nyingi na viatu na chupi kibao na taiti nilipewa akanipeleka kwa sonala nikatobolewa maskio na herein nikavalishwa za gold za kiduara aunta akasema manka we mzuri sana basi tu mamako wa kambo alikua na hila nikacheka kwa aibu na kushkuru sana akasema haya mimi narudi kazini naomba ww sasa uende nyumbn na bodaboda na kuanzia sasa vaa hizo nguo usivae manguo yako hayo utanitia aibu nikacheka nikasema sawa nilirudi nyumbn maisha yaliendelea kipindi hiko nina miaka 14,nilikaa miezi sita nikiishi kwa raha sana nilitakata aunt alinipenda sana aunt aliniambia ana mtoto wa kiume lakini anasoma Kenya na hajaja muda mrefu sana akanionesha na picha zake za zamani akiwa na mwanae nikasema anaitwa nani?akasema anaitwa max nikawa najua hivo. Aaunt aliniambia anataka anipeleke sekondari nikasome mimi nikasema hapana aunt mimi nipeleke ufundi tu mana sina akili za kusoma darasani akasema haya ufundi gani unapenda? nikasema napenda sana kupika na kupamba akasema tena miaka hii hayo mambo yana pesa sana. Sawa nitakupeleka chuo cha ufundi.nikasema sawa nilikaa miezi mingine tukaingia mwaka mppya nikataftiwa chuo nikaanza kusoma nilipata mashosti mbali mbali huko chuoni lakini ushoga ukaiva na msichana mmoja aliyeitwa paula,tulipendana na wote tulikua wapole sana nilisoma kwa raha sana aunt alikua ananipa pesa ya nauli na kula kila siku nilisahau kabisa shida zangu zote nilizowahi kuwa nazo nilisoma miaka mitatu nikamaliza chuo nikiwa na shoga angu kipenzi kabisa paula aunt lola aliniunganisha na rafiki ake aliekua anapika na kupamba kwa tenda nilianza kuwa nae kila akipata tenda nashiriki kupika na kupamba kisha ananipa change kiasi hapo akati nimesha nunuliwa simu na aunt lola na akasema nitunze pesa yeye ataniongezea kidogo vya kununua vifaa vya kupikia na kupambia ili nianze kujitegemea nikasema sawa nilikua na aunt Miriam (mpambaji na mpishi)kwa miezi kama sita kisha aunt akaniambia niende dar kwa rafiki ake mwingine ni mpambaji nikajifunze na fashion za huko zaidi nilifurahi sana akaniombea nikapanda bus hadi dar kisha nikaja kupokelewa na rafiki ake aunt aitwaye mama Diana alikuja na wanawe yeye alikua na watoto wakike wawili mmoja anaitwa felisity na wa pili Diana ambae ndio niliendana nae umri kipindi hiko mimi nina 19 kasoro lakini Diana ana 20 kasoro nilipelekwa hadi kwao mikocheni b na walikua wanazo sana pesa mana kwao kuzuri, na mie kipindi hiko nishakua wa mjini kabisa navaa kisichana haswa nawaka nilipokelewa vizuri sana nilikua naishi kama nyumbn mama Diana alikua anapata sana tenda hivo alikua busy sana na mie kama kawa naenda kujifunza nae nilikaa miezi miwili hapo kupumzika ni siku chache sana nilizidi kujifunza tena nikiwa na Diana, siku moja Diana alimuomba mama yake tukapumzike beach maana hakukuwa na kazi mama yake akakubali basi Diana alichukua gari kisha mimi yeye na dadake tukatoka hadi bahari beach tukalipia na kuanza kuogelea zetu sasa kwa raha mimi sikua fundi wa kuogelea wala nini ivo nilikua nachezea maji tu sehemu fupi mana sijui kuogelea, Diana akasema ww hata hufaidi basi kafate vinywaji huko kaunta nikasema sawa nikatoka majini nilikua na swimming costume yangu na kimtandio bdo kaushamba nilikua nako nikaenda hadi kaunta nilivofika kaunta nikaagiza nikawa nimesimama na simu nasubiri oda yangu mara akaja kaka mmoja akanishika tako nikastuka niaksema ww vipi lione unanishikaje sasa? akasema kwani nini sasa unapiga kelelee kwani bikra wewe?nikasema haikuhusu unikome akasema unalinga eeh ungekua hutaki kushikwa ungetembea hivo matako nje si unatuonesha mmekuja hapa na vimalaya vyenzio kututega si ndio afu ukishikwa unakua mkali ebu tulia uko akawa ananishika kiuno mara kaka mmoja akaja akasema bby kuna nini hapa mbona sielewi akanishika mkono na kunivutia kwake, akanikumbatia afu akasema vipi bro mbona unamgasi mpenzi wangu?yule kaka akasema aah sikujua bro sorry bana akajichekesha akaanza kuondoka, nikamuangalia kaka alieniokoa mmh ni mkaka mtanashati tu anavigezo bana mrefu kiasi hivi nikiwa bado namchora akanikumbatia vizuri akaanza ninyonya midomo,,,uwii nani huyu jmn mbona hivi?.....itaendelea
Comments
Post a Comment