SAM 11


 


"Tuachane na hayo, muda wowote unaweza ukanipigia simu. Mwanvita ametoka muda mrefu eeeh?"

"Ndiyo, kwani anajua kama umekuja huku?"

"Yes! Tuliongea kwa simu"

"Haya sawa" Mage alisogeza kiti karibu na Sam kisha alimuuliza


"Hivi hii kazi inakupa uhuru wa kuonana na wifi yangu?" Tabasamu lilisindikiza swali hili huku macho ya Mage yakiwa usoni kwa Sam ambaye aliinamia chini kisha alitoa jibu baada ya kuinua kichwa.

"Bado sijabarikiwa kumpata"

"Usiniambie umri huo huna demu Sam, au unatumia sabuni kujipoza" aliuliza Mage, Sam alijikuta katika wakati mgumu hakutegemea kuulizwa maswali tata kama hayo tena na Mtu ambaye anafanana na Bosi wake kwa kipato. Alijiuma uma akatoa jibu moja


"Hapana Dada sifanyi hivyo, naamini muda ukifika nitakua naye tu" Mage alicheka kisha akasema

"Rose amekuja ameondoka umemwacha hivi hivi, Bosi wako hana Mume naye umemwacha basi utakua mtakatifu sana wewe" 

"Hao wote nawachukulia kama Dada zangu tu hivyo nawaheshimu sana na siwezi kuthubutu kufanya ujinga, naweza kujikuta nakosa kazi pia" Maongezi yalipamba moto mara honi ya gari ilisikika. Haraka Sam alikimbilia getini kufungua geti, Mwamvita alikua amesharudi kutoka shule alikompeleka Mdogo wake Rose.


Baada ya kuegesha gari, Mage alimsogelea Mwamvita na kumpiga busu matata, Sam aligeukia pembeni na kujifanya hakuona chochote lakini alikua ameona na maswali mengi yalikua kichwani pake. Baadaye alisikia mitembeo, aligeuka na kuwaona wakiwa wanaeleka ndani wakiwa wameshikana mikono.

Comments