Haraka alifungua na kumwona Mwanvita akitapika, alisogea kitandani na kumshika kifua Mwanvita ili kumtuliza Kutapika.
Angalau ilisaidia akawa ametulia akiwa hana nguvu, haraka Sam alifuta yale matapishi pale chumbani huku Mwamvita akimtazama tu Sam, alipomaliza alirudi kitandani kumjulia hali Bosi wake.
"Unajisikiaje sasa Dada?" Aliuliza Sam, Mwamvita alivuta pumzi na kumjibu
"Kiasi niko poa baada ya kutapika, umejuaje?"
"Nilisikia ukitapika Dada"
"Niko sawa unaweza kwenda"
"Sawa Dada lakini kwa lolote usisite kuniita" akisema Sam kwa sauti ya kujali sana, alimfanya Mwanvita atabasamu, ilikua ni mara ya kwanza Sam anamwona Mwamvita akitabasamu
Aliondoka hapo akiwa na furaha sana sababu alimfanya Bosi wake atabasamu, angalau aliona kibarua chake kipo salama sasa.
Asubuhi kulipo pambazuka, Sam alikua amelala baada ya vurugu za Usiku kucha, jumlisha na kufanya mapenzi na Rose. Mwamvita alipomaliza kujiandaa alienda kumwangalia Sam ili afungue geti lakini alimkuta akikoroma, hakutaka kumsumbua sababu alijua tu atakua amechoka, alifungua geti akalitoa gari kisha akalifunga na kuondoka zake.
Rose naye alipoamka hakujua hili wala lile, Mtu wa kwanza kwenda kumtazama alikua ni Dada yake Mwamvita lakini hakumwona, alijua tu atakua kaondoka, akaelekea getini kuonana na Sam, alimkuta akiwa amelala, alimwamsha. Sam aliamka akiwa mwingi wa uchovu
Comments
Post a Comment