SAM 07


 


"Kaka samahani, Mwanvita kalewa sana naomba utusaidie kumpeleka ndani" haraka Sam alisogea hadi upande wa Mwamvita na kusaidiana na Wadada wale wawili, mmoja ndiye aliyekua dereva wa gari ya Mwanvita na mwingine ni ile BMW. Sam ndiye aliyetegemewa sana sababu alikua Mwanaume, alimkokota Mwanvita hadi chumbani na kumtupa kitandani.


"Asante sana Kaka, Sorry Unaitwa Nani?" Aliuliza Mdada mmoja

"Naitwa Sam Dada"

"Ooh Sawa, chukua hii namba kwa lolote utapiga" alisema huyo Mdada, Sam alitabasamu sababu hakua na simu.

"Sina simu Dada"

"Mage nipo nje.." alisema Mdada mwingine ambaye hakutaka kuzungumza sana, akamwacha huyo Mdada anayeitwa Mage akiwa na Sam pale chumbani. 


"Huna simu? Basi utapiga kwa kutumia simu ya Rose, Mwambie ni Dada Mage" 

"Haya sawa" alisema Sam akiwa ameshikilia kadi ya mawasiliano ya Mage ambaye alishaondoka chumbani, Sam akamtazama Mwamvita jinsi alivyo pale kitandani alijikuta akimeza funda zito la Mate kisha akaufunga mlango na kutoka.


Alirudi akafungua geti na kuruhusu ile BMW iondoke, Mage alimuaga Sam kwa kumpungia mkono, Sam alitabasamu sana kisha alirudi kwenye chumba chake kupumzika, ilishagota Mishale ya Saa nane Usiku, akiwa hapo alianza kusikia sauti ya Mtu akitapika, ilikua ikitokea kule chumbani kwa Mwamvita, haraka alikimbilia huko na kugonga mlango lakini ile sauti ya kutapika iliendelea hivyo aliona hakuna sababu ya kuendelea kusubiria.

Comments