Gari ya kifahari aina ya Range Rover ilikua ikiingia ndani ya jumba hilo la kifahari, Samson akiwa na sare za walinzi alikua mwenye wasiwasi sana huku akilifunga geti hilo, mara moja gari ilielekea maegesho. Dakika moja baadaye alionekana Mwanamke mmoja mnene kiasi, mweupe, kwa namna alivyo ilionekana wazi kua alikua ni Mwenye nyumba hiyo. Taratibu alisogea hadi mahali alipo Samson, ilikua ngumu kwa Samson kuhimili presha ya kutazamwa na Mwanamke huyo aliyeonekana kumdadisi sana Samson. Mapigo ya Moyo ya Samson yalikua yakienda mbio sana
"Shikamoo Dada" alisalimia Samson ili kujiondoa katika hali ya woga, miguu ilikua ikitetemeka sana, macho ya Mwanamke huyo yalitua kwenye zipu ya Samson ambayo ilikua wazi baada ya purukushani za kuvaa haraka haraka, alikua kimya hata salamu yake haikuitikiwa.
"Funga zipu yako" alisema Mwanamke huyo huku akionekana kua siriazi sana, haraka Samson aliifunga zipu akiwa anatetemeka na kumeza funda zito la mate. Katikati palikua pameloa na ilionekana kua na ute ute lakini Mwanamke huyo hakuuliza
"Rose yupo wapi mbona simu yake hapokei?" Alihoji
"Itakua ndani Dada maana hajatoka" alijibu Samson huku akikuna kipara chake
"Sawa" alijibu kwa sauti iliyojaa ukakasi kisha akapiga hatua kuelekea ndani.
"Oooh Mungu wangu sijui itakuwaje" alijiuliza Samson huku akimtamaza Mwanamke huyo. Mara moja Nwanamke huyo aliingia ndani na kuanza kumwita Rose
"Abeee Dada" aliitikia Rose kutokea jikoni
"Kwanini hupokei simu yako?" Aliuliza mara baada ya Rose kufika Sebleni
"Dada Mwamvita nilikua na kazi kule jikoni, kila siku nakwambia utafute Msichana wa kazi hutaki, hizi kazi zinanichosha sana" alisema Rose kwa sauti ya kudeka
Comments
Post a Comment