MBWEMBWE ZA FUNDI 26


 


"Una jeuri sana wewe Mtoto sababu ya Mali za Wazazi wenu, unafikiri mali za urithi zinadumu?" Alisema yule Mama akionesha kukereka na mabishano yale yaliyodumu kwa zaidi ya dakika tano

"Mama Lucas hebu tumuache yeye na huyu Kijana maana kazidi kutudharau, Mtu gani ambaye haambiliki?" Alisema Mama mwingine ambaye alikuwa ni Kungwi wa Jolie, wale Wamama wawili waliondoka na kuwaacha Jolie na James pale chumbani. Jolie alifurahi sababu alikuwa akiitafuta sana namba ya James, haraka akamuomba namba James!

"Ahsante! Nakukumbuka sana tokea siku ile Fundi James kila nikikumbuka jinsi ambavyo ulikuwa ukiuchezea mwili wangu napagawa sana" Alisema Jolie akiwa anahema


"Hapana Jolie, hebu jaribu hilo gauni kwanza maana tunaweza kukutwa hapa si umeona zile Nongwa za wale Wamama?"

"Ah! Achana nao Bwana James!!" Jolie alilitupia gauni Kitandani akamwambia James

"Nipe kimoja cha haraka James jamani" Alisema akiwa anamsogelea James pale aliposimama, James alikuwa muoga vibaya mno licha ya utundu wake wote aliufyata Mkia.


"Jolie hapa siyo Bwanaaa wewe unaenda kuwa Mke wa Mtu" Kabla hajamaliza kuongea, tayari Jolie alikuwa ameitupa chini Khanga yake, macho ya Fundi James yalitua kwenye miguu ya Jolie iliyofunikwa na Khanga iliyo anguka.

Comments