MBWEMBWE ZA FUNDI 25


 



Ah! Watu wengine Bwana kuharibiana siku tu, Ok nitampigia nimuulize" Scola aliingia chumbani kwake na Jolie alibakia pale sebleni.


Baada ya wiki moja, James alimaliza kushona nguo ya harusi ya Jolie. Aliwasiliana na Scola akaipeleka nyumbani ili Jolie aijaribu, kitendo cha kumuona James pale kilimtia wazimu akakumbuka jinsi Mwanaume huyo alivyokuwa akiuchezea mwili wake. 


James hakuwa huru pale tofauti na mwanzo akawa anaona aibu hivi hadi Jolie alishtuka. Kulikuwa na Watu wengi pale nyumbani kwao akina Jolie hivyo Scola baada ya kumpokea Fundi James akamuelekeza mahali ambapo Jolie alikuwepo, hakuwa na shaka sababu alipo Jolie kulikuwa na Watu wengine!! Mama mmoja baada ya James kukabidhi gauni za Jolie


"Kaka huruhusiwi hapa ndani kama unavyoona ni Wanawake watupu hivyo nenda nje mara moja" Alisema huku akionesha ishara za vidole

"Jamani huyu ni fundi sasa nani atajuwa kama Gauni liko sawa au haliko sawa? Anapaswa kuwepo hapa ndani"

"Jolie hakuna ruhusa hiyo kwa mila za Kitanzania, vaa gauni kisha ataitwa kuja kuliangalia"

"Hapana Jamani hilo halipo sawa, kwanini mumsumbuwe wakati hilo jambo ni la muda mchache tuu? Tufanye mara moja kisha ataondoka akaendelee na majukumu yake" Kulizuka kutokuelewana kati ya Jolie na huyo Mama, Wakawa wanabishana Jolie akitaka James abakie pale chumbani wakati Yule Mama akitaka James aende nje


Comments