"Hivi wewe huoni kama huyu sio aina ya Wanawake wengine uliowazoea? Hujui kusoma hata picha huoni?" James alipotoka akaongea kwa hasira huku akimyooshea kidole
"Kwani ana Ikulu ya dhahabu? Kajaaliwa Matako tu lakini wakawaida sana"
"Tutakosana mimi na wewe!!"
"Sijali Bwana!! Kwani unafikiria sisikii wivu mimi?"
"Mama Sadiki kwako nilipita tu kwa Bahati mbaya lakini wewe sio taipu yangu" James akaingia ndani akimuacha Mama Sadiki akiwa anacheka na kuimba nyimbo za mafumbo.
Scola baada ya kupata alichokitaka kutoka kwa Fundi James alijisikia raha sana tena mwepesi, hakuacha kufikiria namna ambavyo James alimpa raha.
"Mmh! Sitakubali ule utamu Jolie aupate hata kidogo, nitauwa Mtu haki vile. James jamani Mh!" Alijisema akiwa kwenye gari tayari kurudi nyumbani, hakuoga pale kwa James hivyo alipofika nyumbani akakimbilia bafuni kisha alirudi Sebleni ambako kulikuwa na baadhi ya wageni mbali mbali ambao walikuja kwa ajili ya hiyo harusi ya Jolie na Balozi.
"Simu yako ilikuwa haipatikani Scola, nimekutafuta sana. Vipi hiyo nguo maana siku zilizobakia siyo nyingi!" Aliuliza Jolie kwa sauti ya chini ili wengine wasisikie alichokuwa akizungumza na Scola
"Tatizo lako ndiyo hilo hupendi kuniamini Jolie, nimepewa hiyo kazi sababu najuwa nini cha kufanya" Alijibu kwa malalamiko Scola
"Nimekukumbusha tu wala sina maana mbaya ila kama unaona nimekosea nisamehe" Jolie alisema kisha alikaa wima kama twiga akiwa amenyoosha shingo yake
Comments
Post a Comment