JAMES WA FACEBOOK 16 - 20


 


JAMES WA FACEBOOK 💑 16


Suzy alijaribu kupiga simu lakini alishindwa sababu James aliizima simu yake, mwisho aliona kama James alikua mwongo na hakufanya safari ya kwenda Dar, alichukia sana.


James akafikiria ataenda wapi Usiku huo, hivyo aliona ni bora akazungumze na Suzy, kutokana na kutozoea Maisha ya Dar au kuyajua, aliweka begi pembeni ili amsogelee Suzy, aliponyanyua shingo kutazama alipokua Suzy hakumwona, akaangaza huku na kule akamwona Suzy akielekea nje, akamfwata haraka lakini tayari alishapanda kwenye Tax na kuanza kuondoka


James akatoa simu ili ampigie Suzy, akaiwasha. Alipoiweka sikioni ikakwapuliwa na vibaka walio kwenye pikipiki, James akapaza sauti ya kuomba Msaada lakini hakuna hata mmoja aliyemsaidia, Watu walimpita kama vile hawakumsikia


Haraka akalikumbuka begi lake lenye kiasi cha pesa kilichobakia na nguo zake, aliporudi hakuliona lile begi tena. Watu walikua wengi, Mabasi yalizidi kuingia kwa kasi, wengine walimsukuma James

James akajikuta katika wakati Mgumu sana, hakujua ataweza vipi pambana na Mazingira ya Usiku huo, hakujua atakula nini, atalala wapi, alilia kama Mtoto mdogo



°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°


JAMES WA FACEBOOK 💑 17


Aliketi chini akiwa amepoteza dira, Usiku huo ukawa ndiyo Mwanzo wa Maisha mapya ya James ndani ya Jiji la Dar-es-salaam.


Hadi kufikia saa tano Usiku, James alikua amevimba macho kwa kulia, chozi lilikauka lakini maumivu yaliongezeka. Askari mmoja alimfwata James

“Muda mrefu umekaa hapa unasubiria nini?” alimwuliza, mkononi alikua na Bunduki, hofu na wasiwasi vikazidi kumjaa James, namna alivyo vaa isingelikua rahisi kwa Mlinzi huyo kujiridhisha kua James alikua ameibiwa. Kichwani alikua na mnyoo maarufu wa vijana wa siku hizi, Basi James akaanza kujiliza na kutia huruma


“Hebu simama” yule Askari mwenye Bunduki alimwambia James, haraka James alisimama, yule Askari akamtazama James kwa sekunde kadhaa kisha kwa ukali bila hata kumsikiliza akasema

“Hebu toka hapa stendi haraka sana” James kwa hofu yake akakimbia kuelekea geti la kutokea huku akigeuka nyuma, kwa Bahati mbaya akagongana na Mtu, lakini hakujali akakimbilia nje ili kujiweka salama zaidi. 


Mbele yake palikuwa na Barabara ya Morogoro, hakujua aelekee wapi, kulia kwake ni Morogoro


°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°


 JAMES WA FACEBOOK 💑 18


Alichuchumaa chini huku akilia, akaishika barabara ya pembeni akiwa anaelekea Ubungo bila kujua alikua akielekea wapi.


Alitembea kwa muda mrefu huku usiku ukizidi kua mwingi, mbele aliona kibanda kimoja cha miti ambacho hutumika kuuzia nguo za Mtumba, James akasogea hapo na kujikalisha akiangalia namna Magari yanavyopishana.

“Nimesikia kila kitu na sitaki nikusikie ukiniambia siyo kweli, James nakuonya ukinyanyua Mguu wako hapa na kwenda Dar, nitakulaani” Aliyakumbuka maneno ya Mama yake akiwa anazidi kuvuja chozi, alishapoteza dira ya Maisha


••••••••

Jua lilikua limeshatoka siku ya pili, Mlango wa nyumba ya Suzy uligongwa. Ramla alikua mlangoni ili kusikia kama Suzy alionana na James wa Facebook. Mlango ulifunguliwa, Suzy alikua amevalia khanga nyepesi alimtazama Ramla kwa jicho lililojaa kukata tamaa huku akicheka kwa masikitiko

“Vipi mwenzangu ulifanikiwa kukutana na Handsome Boy?” aliuliza Ramla


“Ndugu, hakuna cha Handsome Boy wala nini. Nayaamini maneno yako, yule mshenzi kala hela yangu na kazima simu. Usikute hata zile picha siyo zake” alisema Suzy, kicheko kikamshika Ramla tena akacheka kwa kujizuia ila akashindwa

“Nilikwambia hukusikia, Wanaume wa Mtandaoni siyo wa kuwaamini kabisa Suzy. Lakini pole Mwaya”

“Nayaamini maneno yako Ramla, yaani yule Mbwa na alaaniwe huko aliko, anafikiria elfu tisini itamfikisha wapi Mshenzi yule” alisema Suzy kwa hasira huku akijisonya


°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°


 JAMES WA FACEBOOK 💑 19


“Haya Mwaya mimi naelekea kazini, Mume wangu ameshaondoka nipo na Dada wa kazi na Mlinzi kama wewe tu” 


“Hahahaha karibu kwenye chama la Upweke shoga yangu” vicheko vikatawala, Ramla akaelekea nje ya Geti akaingia kwenye gari yake kisha akaanza safari ya kuelekea kazini.

Asubuhi hiyo James alikua akitembea maeneo ya Riverside, njaa kali ilikua ikimtafuna, uchovu, hakulala usiku kucha alikua akitazama Magari tu.


 Alipiga mihayo akisubiria magari yaishe ili avuke upande wa pili wa Barabara, hakujua anaelekea wapi ila alichotaka ni kutafuta mahali akae kwanza ili kujipoza na machungu.

Akajikuta anasinzia akiwa amesimama, gari zilipo pungua Watu walianza kuvuka kwa makundi, James alipokuja kuhamaki aliona Watu wanamalizia kuvuka, naye akataka kuvuka bila kuangalia kama kuna gari inakuja.


Bahati Mbaya na lile wenge la njaa, masikini James aligongwa na gari ndogo akatupwa mbele ya gari hiyo iliyofunga breki haraka. Kila mmoja alijishika kichwa, ajali hiyo ilimsababishia James kuvuja Damu.


°°°°°°°°°°°°°′°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°


JAMES WA FACEBOOK 💑 20


Mara moja dereva wa gari alishuka, alikua ni Mwanamke. Dereva alikua ni Ramla rafiki yake Suzy, alipiga kelele za kuomba Msaada. Haraka wasamalia walimchukua James na kumwingiza kwenye gari ya Ramla ambayo ilisababisha ajali, Ramla akaingia ndani ya gari tena nyuma ya gari akiwa anamtazama James aliyeumia vibaya akiwa amepoteza fahamu.

Msamalia mmoja akaiendesha gari ya Ramla kuelekea Hospitali jirani. James akaanza matibabu, Ramla hakwenda tena kazini siku hiyo, akampigia simu Suzy kumpa taarifa ambapo Suzy alifika Hospitali mara moja baada ya kupata simu ya Ramla.


●●●●●●●●●●●●

Alimkuta Ramla akiwa analia jicho jekundu sana 

“Masikini pole, ni mzima?” 

‘Sijui Suzy, amepelekwa chumba cha wagonjwa mahututi, nimechanganikiwa sana, kama amefariki itakuaje kwangu?” alisema Ramla akiwa anazidi kulia, Suzy akamkumbatia Ramla

“Usijali atakua sawa” 


Hadi jioni inafika Suzy na Ramla walikua Hospitalini wakisubiria majibu ya Mgonjwa wao, wakati giza linakaribia ndiyo Daktari alivyotoka chumba alicholazwa James, haraka Suzy na Ramla walisimama

“Dokta anaendeleaje?” aliuliza Ramla kwa hofu

“Usijali, mgonjwa anaendelea vizuri, alipata tu hitilafu kichwani lakini sasa yuko sawa”

Comments