MBWEMBWE ZA FUNDI 15

 



Ndani ya gari ya kifahari aina ya TOYOTA FOX Scola alikuwa akikumbuka alichokifanya ndio maana aliiacha flash kwenye TV bila kuichomoa, alichokifanya ni kufuta kila kitu ili usibakie ushahidi wa aina yoyote ile. Alifanya hivi ili kumuondoa wasiwasi ndugu yake, Scola baada ya kuwaona James na Ndugu yake wakiwa katika hali za kushangaza chumbani alihisi uwepo wa jambo la kimapenzi kati ya Watu hao wawili ndio maana akaamuwa kuharibu kabisa ile video.


"Jolie! Wakati huu huwezi kunishinda" akasema kwa sauti Scola huku akiendelea kukanyaga mafuta akionesha kuficha jambo fulani lililopita!! Ni mwendo wa masaa matatu alikuwa akiweka gari vizuri mbele ya ofisi ya James lakini cha kushangaza alikuta ofisi ikiwa imefungwa. Akapata wazo la kumpigia James lakini simu haikupatikana, Ndipo akaulizia Kwa mtu mmoja ambaye alikuwa akiuza matunda karibu na ofisi ya James!!

"Samahani naulizia mahali anapoishi James kama unapafahamu, simpati kwenye simu" aliuliza akiwa ana tabasamu ili kumtoa wasiwasi yule jamaa ambaye alionekana kushtuka kidogo

"Anhaa!! James anaishi pale mbele, ukienda na hii barabara, kata mtaa wa pili alafu ulizia hapo ila tumia jina la kifurushi ndio utampata"

"Kifurushi?"


"Ndio, james ni maarufu sana kwa jina hilo mtaani kwao. Ukiuliza James humpati Dada yangu" kwa maelezo haya, Scola akarudi kwenye gari ili afuate alichosema muuza Matunda. Alipofika mtaa wa pili akamuulizia James kwa jina la kifurushi, akampata Mtu akamsindikiza huko kwa kutembea.


Kila aliyepishana na Scola alisimama ili kuangalia ni namna gani Mungu aliifanya kazi ya kumuumba kikamilifu sana, mguu wake ulikuwa umekatika, gauni la kitenge alilolivaa lilikuwa likicheza kila alipopeleka mguu mbele!!

"Nyumba ile pale" Mtu wa kusindikiza akaonesha mahali ambapo James alikuwa akiishi, akavuka kidaraja kidogo hadi nyumbani anakoishi James!!

Comments