Aliyekuwa anamuoa Jolie alikuwa ni Mwanaume wa makamo wa miaka 55 ambaye alikuwa akielekea kwenye uzee, alikuwa na pesa za kutosha na ndizo zilizo mfanya Jolie akubali kuolewa naye wala hakumpenda, alikuwa danga lake kwa zaidi ya miaka mitatu hatimaye ndipo akataka kumuowa.
Taratibu nyingi za harusi zilikuwa zikifanyika, kila mmoja alisimamia jambo aliloombwa kulisimamia. Wa chakula alihangaikia chakula, wa mavazi, ukumbi, na mambo mengine walikuwa bize kwenye majukumu yao!!!
Baada ya kikao kifupi, Scola akamuaga Ndugu yake kuwa anaenda kuangalia maendeleo ya nguo kwa fundi James, meseji aliyoituma haikupata kujibuwa na James hivyo akawa na wazo la kwenda kuongea naye ana kwa ana ili amwambie shida yake. Moyo wa Jolie ukawa na mashaka sana akakumbuka kuhusu Flash ya gari, Scola alipoondoka alisahau kuitoa kwenye TV.
Wakati Scola anawasha gari, Jolie akautumia mwanya huo kuingia chumbani kwa Dada yake kisha akaichukuwa Flash na kurudi nayo chumbani kwake, aliposikia geti likifunguliwa akaenda kuchungulia dirishani akamuona Scola akiwa anaondoka pale nyumbani kwao.
"Lazima nijuwe Scola" akasema huku akiwa anachomeka Flash kwenye TV
Akashangaa kuona ndani ya ile Flash hakukuwa na kitu hata kimoja ambacho angeweza hata kuangalia
"Si alisema kuna movie humu mbona hamna kitu" akajiuliza akiwa amejishika kiuno chake
"Ananificha kitu gani?" Akajiuliza tena kisha akairudisha ile Flash kwenye TV ya Scola, hakufanikiwa kujuwa wala kuona video ya James!!
Comments
Post a Comment