"Helllo" James akapokea simu ya Scola
"Vipi umemaliza?" Aliuliza Scola akiwa ndani ya gari mara baada ya kumaliza kuangalia video zilizorekodiwa na kamera ya ndani ya gari, akachukuwa Flash ya kumbukumbu akaitia kwenye mkoba wake.
"Bado kidogo Scola ndio namalizia"
"Eeeh kwani unapima watu 10 James?" Scola akatoka kwenye gari, sauti ya kufunga mlango ikasikika na simu ikakatika.
"Dada yako anakuja"
Mara moja Jolie akavaa khanga yake, wakaendelea na vipimo, Scola alipoingia akawakuta wakiwa wanaendelea kupimana pale chumbani.
"Nimeshamaliza" akasema James, Scola alipotupa macho yake kwenye msuli wa James akaona kama maji maji hivi, akamtazama na Jolie akaona nywele zake zikiwa Tim tim.
"Nini kimeendelea hapa?" Akajiuliza ndani ya akili yake Scola, akawa amekosa jibu la moja kwa moja.
"Twende nikurudishe James!" Akasema Scola
"Si ungemuacha apumzike kidogo Dada! Huoni kama atakuwa juu juu sana?" Akadakia Jolie na kumfanya Scola aingiwe na mashaka
"Aaah! Usijali nina wateja Kwahiyo natakiwa niwahi kurudi alafu pia nina kazi ya kutafuta Material kwa ajili ya Nguo yako Jolie" Akasema James baada ya kuona sura ya Scola ikiwa kwenye hali ya wasiwasi.
"Ulisema utanirudisha vile?" Akauliza James ili kuondoa hali ya aibu aliyokuwa nayo, wanasema mwizi ataendelea kuwa na wasiwasi hata kama hakufanikiwa kuiba
Comments
Post a Comment