MBWEMBWE ZA FUNDI 04

 



Fikra za James zilisababisha aanze kubana miguu yake ili kuzuia Joka lake lisionekane maana tayari msuli ulikuwa umeanza kutuna, Scola akaanza kushangaa baada ya kumuona James akiwa amebana miguu, akahisi labda James anaumwa, akasimamisha gari pembeni

"Fundi James unaumwa?" Akauliza Scola pasipo kujuwa kuwa paja lake lilikuwa ndio Ugonjwa wenyewe ambao Fundi James alikuwa akiumwa

"Hapana niko sawa Scola, hujanizoea ndio maana"

"Mhhh! Au nizime AC"

"Hapana kwanini uzime iache tuu"


"Basi ngoja nikununulie maji ya Baridi" Scola akachukuwa Pesa kwenye waleti yake, akashuka ili kumnunulia Maji Fundi James, aliposhuka na kufunga mlango James alihema kama vile Panya aliyenusurika kuuawa na paka.

Akaitoa mashine yake ndefu nene iliyojaa kwenye chup, akaizungusha na kuirudisha ndani ya Chup yake. Dakika moja baadaye Scola akawa amerudi,


"Maji haya hapa, ukijisikia vibaya niambie" Akasema kisha akampa maji Fundi James, akawasha gari wakaendelea na safari ya kuelekea Mikocheni

"Huwezi amini nimeangaika sana jinsi ya kupata fundi anayejuwa hasa kushona maana ni harusi ya mdogo wangu anaolewa na Balozi wa Tanzania ambaye anaishi Uholanzi"

"Ooh!! Kwahiyo wanaenda kuishi Uholanzi?"

"Hapana wataishi hapa hapa Tanzania kwasababu Balozi anastaafu miezi miwili ijayo"

"Hiyo harusi itakuwa kubwa mno"

"Ndio maana sikutaka kumuangusha kwenye mavazi, kukupata wewe ni faraja kubwa kwangu" Maongezi yao yaliendelea huku safari ikizidi kupamba moto na sasa walikuwa mataa ya Magomeni

Bado nguo ya Scola iliendelea kujivuta vuta japo alikuwa akijitahidi kujiweka sawa lakini hakufanikiwa kuziba macho ya Fundi James yasione uhalali wa mlaji kwenye paja la Scola.

"Wewe harusi yako imepita?" Akauliza Fundi James kwa mtindo wa masihara tu kumbe alikuwa akimaanisha alichouliza, akamfanya Scola aanze kucheka kisha akaachia tabasamu

"Kwanini umeuliza hivyo?"

"Ni vibaya nikijuwa?"

Comments