MBWEMBWE ZA FUNDI 03


 


"Naitwa Scola, nimeulizia sana kwako lakini bahati mbaya simu yangu ilizima." Alisema akiwa ameketi kwenye sofa dogo la kupokelea Wateja

"Oooh! Pole sana lakini umeshafika na umenikuta" Alisema Fundi James huku akitupia macho yake kwenye mguu wa Mwanamke aliyejitambulisha kama Scola

"Nahitaji kushonewa nguo za harusi, nimeona nguo zako kwenye mtandao wa Instagram. 


Nimependa ubunifu wako" Akasema Scola huku akiwa anatoa paswedi kwenye simu yake kubwa aliyoishikilia mkononi

"Mshono ni huu hapa" Akampatia simu Fundi James ili auangalie

"Huu unawezekana"

"Gharama zake? Nahitaji tatu kama hizo"

"Kila moja ni laki tatu lakini kama material ni yako itakuwa laki mbili na nusu"

"Sio tatizo, sasa anatakiwa kushonewa Bibi Harusi na yupo nyumbani, tunaweza kuongozana mara moja ukampime?"

Fundi James akakaa kimya kidogo akionekana kutafakari kisha akamwambia

"Tukimbie mara moja" Wakaingia kwenye gari kisha safari ikaanza

Gauni alilovaa Scola lilikuwa fupi hivyo alivyokaa kwenye usukani akajikuta mapaja yake yapo nje nje, kama ilivyo kwa Wanaume wengine James akatupia jicho mara moja akalitazama paja la Scola lililokuwa limekaa kihasara hasara, akajikuta akikohoa tuu

"Vipi fundi nizime AC unajisikia vibaya?"

"Hapana ni Bahati mbaya tu niko sawa"


Mguuni Scola alikuwa amevalia kikuku cha Almasi, ilitosha kumpa taarifa James kuwa alikuwa ametoka kwenye familia yenye hela kweli kweli. Kila Fundi James alipotupia macho kwenye mapaja ya Scola alijikuta akianza kuingiwa na hisia za kimapenzi, jinsi gauni lilivyokuwa linajivuta taiti nyeupe ilianza kuonekana na hapo ndipo James aliposhindwa kujizuia. Akatamani amwambie kuwa akae vizuri lakini akaona ataonekana bwege endapo atamueleza hivyo

Comments