Alikuwa akiishi maeneo hayo hayo ya karibu na ofisi yake, alikuwa Mkweli na mwenye kutimiza ahadi Kwa Wateja wake.
"Hakuna fundi wa kumzidi James kwa Tanzania hii, jamaa ni fundi sana anajuwa mnoo" Yalikuwa ni maneno ya baadhi ya Watu kwenye vibanda vya kupigia stori, hasa vya kahawa
"Mnayosema ni kweli lakini sio bure uchawi unachangia"
"Kama Uchawi ndio biashara basi kila Mtu angekuwa Mchawi ili afanikiwe katika Biashara, yule ana kipaji"
"Naona anacheza cheza tu na Wake za Watu hana lolote" ilikuwa ni kawaida kuwasikia Watu wakimzungumzia Fundi James ambaye alikuwa ni Kijana tuu.
Siku moja akiwa kazini alisikia mlio wa gari, alipogeuka akaona Gari nyeusi ya kifahari sana ikiwa imesimama nje ya Ofisi yake, hakuna aliyeshuka kwenye gari. Kwakuwa ilikuwa imesimama mbele ya ofisi yake, James akaelekea kusikiliza.
Mara akaona mlango ukifunguliwa kisha akashuka Mwanamke mmoja wa makamo, kwa kukadilia anaweza akafika kwenye miaka 40 hivi na kwa jinsi alivyoonekana alikuwa ametokea kwenye familia yenye pesa haswaa, Alikuwa mweupe mwenye mguu wa Bia, kifuani ilikuwa ngumu kukadilia ila alikuwa amejaza vizuri, nyuma alikuwa amefunga tela la maana. Fundi James akashusha miwani yake ili kuutazama ufundi wa Mungu
Yule Mwanamke akatabasamu akiwa anasoma bango lililo tundikwa mbele ya ofisi ya James, alionekana kuwa mgeni na ni wazi kuwa alikuwa amefika pale kwa kuulizia sana, akamtazama Fundi James akamuuliza
"Wewe ndio Fundi James?" Akauliza kwa sauti ya mbali
"Ndio ni mimi" akajibu James sababu alishazoea kutembelewa na Wateja wageni na kilichomtabulisha yule Mwanamke kuwa huyu ni Fundi James ni vifaa ambavyo James alikuwa ameshika ikiwemo kipimo cha nguo
James alipofahamu kuwa Mwanamke yule alikuwa akija ofisini kwake basi akarudi ofisini ili kumpa nafasi yule Mwanamke amfuate, jinsi alivyokuwa akitembea alionekana kuwa umbo lile lilikuwa likimpa shida wakati wa kutembea, basi naye akafanikiwa kuingia ofisini kwa James, siku hii hakukuwa na Mtu mwingine zaidi ya James pale ofisini.
Comments
Post a Comment