James ni fundi kushona, ni fundi maarufu sana maeneo ya Tandika. Watu wengi hupendelea kwenda kushona nguo kwake kwasababu anajulikana kwa ustadi wake wa kushona nguo za kisasa, Mara nyingi hushona zile nguo za kike na kuziweka kwenye mtandao wa Kijamii. Humfanya apate pesa nyingi kutokana na umahili wake wa kushona, Licha ya kuwa bado ni Kijana wa miaka 28 tu lakini mara nyingi hupendelea kuvaa msuli, Watu wengi hufikiria tofauti vazi la James hadi kupelekea wengine kusema ni mchawi na wengine husema pengine ana Busha ( Mshipa )
Jina lake na mavazi aliyokuwa akiyavaa havikuendana kabisa, mavazi haya huvaliwa na Watu hasa wa Visiwani huko na huaminika wengi wao huwa na Busha, ukiachana na Msuli aliokuwa akiuvaa pia alikuwa akivaa kikoi na Barakhashia juu yaani ukimtazama unaweza fikiria ni Watu wa Visiwani huko tena wale wanaonukia Karafuu kumbe ni Mtu wa Dodoma maeneo ya Mkuhungu.
Ofisini kwa James huwezi kukuta Mwanaume zaidi ya Wasichana na Wanawake wa aina tofauti tofauti ambao ndio walikuwa Wateja wake wakubwa, ucheshi wake ulimfanya apendwe sana na Wadada lakini hakupenda sana alipokuwa akiulizwa kwanini alikuwa akivalia msuli kila siku tofauti na Wanaume wengi ambao huvaa Suruali wanapokuwa Makazini au hata kwenye matembezi.
Ukitaka kumkera James muulize kuhusu Msuli ndio maana wengi wakaweka dhana kuwa huenda James ana Busha na wengine huenda mbali kwa kusema ni mchawi ndio maana anapata wateja wengi sababu ya vazi hilo.
Comments
Post a Comment