UTAMU WA DADA NAA 19


 



Kweli wewe ni Fundi dogo.. Hongera sana.. Hii kazi utaiweza.. 

Haya inuka turudi eneo la Mazoezi.. Nadhani umeshajitambua wewe ni nani.. Umeshatambua upo wapi na unaenda kuwa nani.. 

Aliongea Mzee na kumshika mkono Saidi kisha kuondoka nae.. 


ENDELEA.... 

Kwa namna moja ama nyingine. Saidi alikuwa amepata nguvu kidogo ya kufanya kazi kubwa na ngumu kama ile.. 

Hakuwa na pingamizi wala kigugumizi tena cha kufanya maamuzi kama Mwanzo.. 


"" " Kama Nasra aliweza je mimi ni nani nishindwe.?? Kama madam Rehema aliweza Mazoezi magumu kama haya je mimi ni nani nishindwe.?? 


Waswahili husema.." "" "Kisicho kuua basi hukukomaza.." "" Naamini na mimi pia naenda kukomaa.. Nitakuwa mwingine na mwenye uwezo mwingi zaidi.. 

Eeehh Mwenyezi Mungu nisaidi mimi.. 


Aliwaza Saidi huku anapiga hatua za haraka haraka kufuatana na Mzee kuelekea kwenye Gari.. 


Walipanda Gari na Safari ya kwenda Bondeni ilianza.. 


Wao walizoea kupaita Bondeni kule chini ya Ardhi kwasababu pako chini..


Walifika na Saidi alikabidhiwa kwa wale wale Askari akiwa bado amevalia koti lake la kijeshi alilopewa na mzee.. 


Baada ya Saidi kukabidhiwa pale.. Yule mzee aliondoka bila ya hata kuaga.. 


******

"""" Dogo unaraha sana.. Yaani umekuja leo tu basi umeshakuwa rafiki na bosi hadi anakupeleka kambini.. 

Ujue nyota yako ni nzuri sana.. Wenzio tangu tumeingia humu hatujawahi kutoka na kwenda kambini wala hatujawahi kuliona jua kwa zaidi ya miaka kumi... 


Kweli kabisa ni mwaka wa kumi sasa tupo chini huku kutoa elimu kwa maaafisa wapya mnaokuja kama nyinyi.... 


Hakuna mwenye simu wala hakuna mwenye  Mawasiliano na nyumbani kwao... 


Tupo tu tunashangaa humu na hatujui kama ndugu zetu wapo hai au wameshakufa hadi leo hii.. 

Aliongea mmoja wa wale Maafisa wanaotoa mafunzo... 


Walikuwepo maafisa watatu kwa muda ule, walikuwa na umri kama unalingana hivi na walionekana ni watu wenye kupendana na kuheshimiana sana.. 


*****

"" "" " Kwanini sasa mnafanyiwa kitu kama hiki..??? 

Saidi aliongea Kwa upole na kuketi chini kwenye Nyasi na kuanza kuwatazama bila hofu hata kidogo.. 


***

" "" Dogo Saidi.. Sisi tulikuwa vijana wadogo tu kama wewe.. 

Enzi hizo tulikuwa tunasoma chuo kikuu cha Dodoma mwaka wa Kwanza 2007.. Hii ilikuwa ni baada tu ya chuo kile kufunguliwa Rasmi na Mheshimiwa Raisi pamoja na Waziri mkuu wa wakati ule... 


Tulianza masomo tukiwa kwenye hali ngumu sana na tulikuwa wanachuo wengi kupi kiasi... 

Mazingira hayakuwa mazuri kupata huduma kama chakula na maji pamoja na kituo cha Afya.. 


Hali ile ilipelekea wanafunzi tuandamane makundi kwa makundi.. 


Mimi na wenzangu hawa wawili ndio tulikuwa waanzilishi wa Mgomo na maandamano yale... 


****

Baadhi walikufa na baadhi walipata ulemavu wakudumu, 

wengi walifukuzwa chuo lakini sisi waanzilishi wa mgomo ule, tulikamatwa na watu wa usalama kuingizwa kwenye jengo moja Kubwa sana pale chuoni, Kinaitwa Chimwaga Hall.. 


Tuliingizwa kwenye chumba fulani cha Siri sana. Chumba chenye giza kupita kiasi. Hata kuonana sura tulikuwa hatuonani mimi na wenzangu.. 


Tulikuwa tukisikilizana kwa sauti tu.. 


Huko tulikaa kwa masiku kadhaa bila kujua Upi ni mchana na upi ni usiku.. 


Hatukujua chochote kinachoendelea uraiani. 


Tulikaa kwa masiku kadhaa na baadae tulitolewa kwenye mazingira yale ya Giza na kupelekwa kwenye chumba fulani chenye Mwangaza.. 


Kidogo ilikuwa ahueni kwasababu tulichoka kukaa kwenye Sero yenye Giza ambapo tulikuwa tukila na kunya humo humo.. 

Muda mwingine tulikuwa tukikanyaga au kulalia mavi yetu wenyewe.. 


Kiukweli yale yalikuwa ni mazingira Magumu kuwahi kuishi tangu nimezaliwa.. 

Siwezi kusahau milele.. 


Aliongea yule kaka... 


******

Baada ya kutolewa mule Sero na kupelekwa kwenye chumba cha wazi.. 


Walikuja wadada wanne walio valia nguo za jeshi na kutuvua nguo zetu zote na kila mmoja alibaki uchi kama alivyo zaliwa... 


Walichukua nguo zetu na wawili walienda kuzifua, 

kisha wawili walituingiza bafuni na  kutuogesha.. 


Tulitoka tukiwa wasafi na kuletewa nguo zetu zikiwa zimeshakauka na zilikuwa zimenyooshwa vizuri sana.. 

Tulivaa na kupuliziwa pafum kidogo kisha kutolewa kwa mlango wa nyuma wa jengo lile na kupakiwa kwemye Gari Fulani jeusi na lilikuwa na Vioo vyeusi sana pia.. 


ITAENDELEA...

Comments