"" Alikuwa anaitwa Madam Rehema... Kwa sasa Dada yule yupo njiani anaelekea nyumbani kwako kaitwa na Nasra..
Aliongea yule mzee na kuzidi kumshangaza Saidi..
Kumbe Reheme Alieitwa na Nasra ili wakampe kipondo Dalali Sele ndie alikuwa Mwalimu wa Saidi shule ya msingi na anamjua kitambo tu...
Saidi aliendelea kushangaa sana maajabu yale.. Saidi alikumbua kweli alikuwa anapendwa sana na Madam Rehema na muda mwingi alikuwa akimuita hata akamchinjie kuku nyumbani kwake.. Au hata kunywa chai muda wa mapumzika na kadhalika..
Na kweli saidi alishawahi kumtia mwalimu yule pia... 😂😂😂
Saidi alishaanza ngono kitambo tu sema alikuwa Simba mwenda pole... Anakula na kutulia kimya bila mtu kujua..
********
"" "" Naamini Umeanza kuelewa dogo kwa kukupa ufupi huo wa watu walio kufuatilia au unataka tukupe zaidi.???..
Aliongea Mzee...
Saidi yeye hakujibu kitu alibaki kumtazama tu mzee bila kummaliza.. Hakuamini kabisa kusikia habari zile alihisi huenda anaota...
*
"" "" Unamkumbuka Dereva boda boda rafikiako sana alikuwa anaitwa Alex pale kijiwenu kwenu.
Mkaka mmoja mchafu mchafu sana na anapenda kulewa pombe kali na anavuta sana sigara...
Yule dogo alikuwa anakulinda na kukufuatilia kwenye kila hatu wakati ukiwa kwenye kituo cha boda boda..
Naamini ndie rafikia yako mkumbwa na ulikuwa unampa siri zako nyingi hadi ile siri unayo itunza sana kuwa wewe si mtoto wa mzee Juma bali baba yako ni mmoja wa viongozi wakubwa tu nchi hii kwa sasa..
Ulimweleza pia kuwa kweli huwa unawasiliana na baba yako mara nyingi tu na alikuomba ufiche siri kuwa wewe ni mtoto wake wa kambo ili kulinda hadhi yake..
Hata kampuni ya bahati na sibu uliyoshinda ilikuwa ni mali ya baba yako..
Aliwaambiwa wakupe ushindi ili upate pesa za kuanzia maisha kwa njia hiyo ili watu wasikushtukie wewe wala wasimshtukie yeye..
Hata siku ya kuchukua zawadi ulikabidhiwa na baba yako hundi ile watu wakiwa wanashangaa tu bila kuelewa....
Aliongea yule mzee...
Muda huo Saidi alirudi nyuma na kushika kiuno baada ya kusikia Siri zake kubwa na nzito zinazidi kumiminwa...
"" " Ama kweli usimpe siri zako kila mtu.. Unaweza kumwamini Rafiki kumbe ni mtu anae kuchunguza...
Aliwaza Saidi huku anamtazama yule mzee...
" "" "* Usishtuke dogo.. Rudi ukae tu.. Huwezi kwenda popote, hapa tupo katikati ya kambi ya jeshi. Hakuna pakutokea hata ukitoroka huwezi kwenda popote...
Aliongea Mzee...
Saidi alishusha pumzin na kurudi kukaa..
*******
" "" Dogo hadi Nasra tulimtuma kukuchunguza wewe.. Achana na habari za akina Dalali seke na usanii wake wa kuwatapeli hadi maafisa bila kujua..
Kwasasa Sele anaumia huko kwako. Yupo Nasra na Rehema wanampa kichapo...
*****
"" " Dogo.. Nasra hawezi kuwa mke wako.. Mume wa Nasra ni Tanzania.. Leo hii muda wowote akitumwa kazi atatoka kwako na kwenda kuolewa na mtu kwaajili ya kumchunguza..
Sasa huoni kama ni mke wako utateseka.???
" " Wewe pia mkeo ni Tanzani.. Na muda wowote ukiagizwa ukamtongoze fulani ukalale ndani kwake na umchunguze utapaswa uende, haijalishi ni mwanamke gani...
Aliendelea kuongea Mzeeee..
Saidi alikuwa anatumbua tu macho muda wote...
******
"" "" Dogo Saidi..
Nasra alikuja ili kukuunganisha Rasmi wewe uingie kwenye mikono yetu.. Nashukuru kafanikisha..
"" " Muda wote unao jidai wewe ni kichaa.. Nasra alikuwa anakujua vyema tu na alikuwa nakuchunguza kujua ni kiasi gani unaweza kuigiza.
Kweli wewe ni Fundi dogo.. Hongera sana.. Hii kazi utaiweza..
Haya inuka turudi eneo la Mazoezi..
Nadhani umeshajitambua wewe ni nani.. Umeshatambua upo wapi na unaenda kuwa nani..
Aliongea Mzee na kumshika mkono Saidi kisha kuondoka nae..
ITAENDELEA....
Comments
Post a Comment