ILIPOISHIA.....
"" "" Sikiliza Sele. Katika watu watatu unaokutana nao kwenye Jiji hili la Dodoma.. Basi ujue mmoja kati yao ni mtu wa ulinzi na usalama..
Haya ni makao makuu ya nchi.. Humu kuna hazina ya Nchi.. Humu kuna siri za nchi..
Kuwa makini utakuja kufa sawa..
Aliongea Nasra na kusogea Mezani kuchukua Simu yake kumpigia Rehema..
********
"" " Halo Shosti.. Umeshamkamata huyo ng'ombe.?? Aliongea Rehema mara tu baada ya kuipokea simu...
" "" Ndio shost njoo home mara moja...
Aliongea Nasra na kukata Simu....
********
********
********
Huko kwenye viwanja vya kazi Saidi alikuwa anamalizia kula huku akiwa hajielewi imekuwaje hadi ameingia kwenye majukumu yale..
Baada ya kumaliza chakula..
Yule mze aliempokea Saidi kwa mara ya kwanza alikuja na kusimama karibu kabisa na Saidi..
Saidi aliinua Uso wake na kumtazama yule mzee kwa huruma..
""" Naomba nisaidie baba nitoke humu...
Aliongea Saidi kwa upole sana huku anamtazama yule mzee...
Mzee alimshika Saidi mkono na kuondoka nae..
Walietembea kule chini na kukuta njia moja zinapita gari ndogo ndogo za kijeshi.. Yule mzee alisimamisha moja ya zile gari na kupanda akiwa na Saidi.
Njia nzima mzee hakuwa anaongea chochote..
Gari lilitembea kwa umbali fulani hadi likafika sehemu na kuanza kupanda kama mlima kisha kutokea kwenye Ardhi ya juu.. Gari lilipaki katikati ya majengo fulani makubwa na kila pande kulikuwa kunalindwa na Wanajeshi...
Kumbe muda wote walikuwa Under Ground au chini ya Ardhi kwa maana ingine..
Sasa muda huu walitoka njee na kutokea katikati ya kambi ya Jeshi...
Hakukuwa na upenyo hata kidogo wa saidi kutoka pale..
Mzee alishuka na Saidi akiwa amemshika mkono vile vile na kuingia nae kwemye moja ya chumba kwenye majengo yale....
Walifika na mzee alichukua koti lake la kijeshi na kuvaa kwasababu kulikuwa na Baridi sana...
Aliinuka na kufungua kabati fulani na kutoa koti jingine na kumrushia Saidi..
Saidi aliidaka na kuitazama kisha kuivaa...
"" "" Have a seat.. ( kaa hapo)) aliongea mzee na Saidi alikaa..
"" "" Dogo unaitwa nani.?? Taja majina yako kamili na usinitajie namba kama ulivyo fundishwa kule..
"" " SAIDI JUMAA. aliongea saidi kwa upole huku anaitazama tazama koti la jeshi aliyoivaa.
" "" Saidi karibu.. Wewe ni mtoto wa Tanzania.. Baba yako ni Tanzania.. Mama yako ni Tanzania, Dada na kaka yako ni Tanzania. Mke wako pia ni Tanzania..
Ukiwa mtanzania basi hupaswi kuchagua nini chakufanya kwasababu wewe ni mali ya Serikali ya Tanzania..
Muda wowote ukihitajika kulitumikia taifa uwe tayari tena kwa nguvu zote na kwamikono miwili.. Hakuna kauli ya kipumbavu na isiyo faa kutamkwa huku kama kuomba kurudi uraiani.. Kwani wewe ni mgonjwa..
Alafu huo ni umama unauleta humu.. Ukipewa nafasi kama hizi shukuru na uingie kuitetea nchi yako uandikwe kwenye vitabu vya mashujaa wa nchii..
Hembu acha utoto sawa Dogo..
Aliongea Yule mzee na Saidi aliitika kwa kutikisa tu kichwa kuashiria amemuelewa..
"" "" Dogo hatujaanza kukufuatilia wewe leo au jana..
Yaani Kuanzia wewe ni mtoto tulishaanza kukuchunguza..
********
"" " Unakumbuka kuna siku ukiwa shule ya msingi uliwahi kucheza mchezo ya kuigiza na wenzio halafu ukajidondosha na kujidai umekufa.
Watu waliamini kuwa umekufa hadi wazazi wako walikuja na daktari alikupima na kusema kweli umekufa kumbe ulikuwa unaigiza tu na baadae uliinuka na kuanza kucheka.!!!!
Aliongea Yule mzee....
Saidi alishtuka na kukaa vizuri baada ya kusikia habari zile za tangu akiwa mtoto mdogo shule ya msingi..
Alikumbuka siku hiyo na kweli alichapwa sana na walimu na wazazi pia baada ya kufanya utani kama ule..
*******
"" "" "Basi Enzi hizo tulianza kukufahamu na tulikupenda kwa utaalamu wako ndipo tulianza kukufuatilia...
"" " Ukiwa unasoma Shule kuna mwalimu mmoja alikuwa akikupenda sana na hata mda mwingine alikuwa akikuita kwake kunywa chai hadi wenzio wakaanza kukusema kuwa unatembea na mwalimu wako ukiwa darasa la Saba..
Basi mwaliu yule alikuwa mtu wetu na alikuwa na jukumu la kukufuatilia kwa ukaribu zaidi..
Comments
Post a Comment