UTAMU WA DADA NAA 13


 


ILIPOISHIA.....

Aliongea Nasra na kumfanya Saidi akae kwanza vizuri kwenye Kochi na kuanza kumtazama Mpenzi wake.. 


Saidi aliogopa sana hadi alikuwa anaaza kutetemeka kwa hofu.. 


"" "" Huyu binti kaifungia kamera nyumba yngu au.. Alijiuliza Saidi huku anatazamana na Nasra  


"" "" Hapana Saidi hata usije kuhisi kama mimi nimefunga kamera kwako.. Sijafunga chochote lakini nakuomba tu utambue uwezo wangu.... 

Aliongea Nasra.. 


Saidi alishtuka zaidi na kubaki anatumbua tu macho.. 


"" " Au ni jini huyu dem.. Aliendekea kuwaza Saidi.. 


Saidi akiwa bado haelewi nini cha kufanya.. Alishangaa amesogelewa zaidi na Nasra kisha akashikwa kichwa na kukutanisha Ndimi zao..


" "" Najua unafanya yote kwasababu unanipenda na unapima usahihi wangu kwako..

Jiamini Mwanaume, mimi nikipenda huwa napenda haswaa. Hata usiwe na Shaka...


Lakini Mchezo wako nimeuelewa sana kipenzi... Unafaa sana kwenye kazi kama zetu...


"" "" Mmmhhhh.. Nafaa vipi sasa wakati mimi sijasoma jamani.?? Elimu yangu ya Msingi tu.. Aliongea Saidi na kujisahau kama alikuwa Kichaa 😂😂😂"" ""


"" "" Kumbe siyo kichaa kweli. Maana mimi mwenyewe nilikuwa nabahatisha tu hapa. Ungeendelea na Uchizi wako wala hata nisinge jua.. 


Siunaona hiyo bahasha hapo mezani.. Nilikopa pesa benk ili nikakutibu..


Afadhali umeiokoa pesa hii... Basi uichukue ukaongezee kwenye biashara zako mpenzi... 


Deni nitaendelea kulilipa tu mimi mwenyewe watanikata mshahara wangu...


"" " Saidi, naomba utambue pia kuwa nakupenda na nimekuridhia jinsi ulivyo.. Nimekupokea kwa kila namna.. Sina pingamizi na wewe.. Nimekupa pesa hizo kukudhihirishia kuwa sihitaji pesa zako...


Mimi napokea Mishahara miwili kila Mwezi tena mikubwa tu.. 

Usijali kuwa na amani.. Lakini ukiwa na mimi utambue tu majukum yako ya kuisimamia familia kama Mwanaume, kwasababu ni majukumu yenu. 

Ikitokea umekwama basi niambie hata usiwe na wasiwasi..


ALIONGEA Nasra na kuinuka kuingia chumbani..


Saidi pia aliinuka na kumfuata mpenzi wake kwa nyuma..


Aliingia pia chumbani na kumkuta mpenzi wake anavua nguo ili ajilaze kitandani....


"" "" " Nimechoka baby.. Naomba kupumzika.... Aliongea Nasra....


Saidi aliitika kwa kutikisa kichwa huku anavua pia nguo na kujilaza karibu kabisa na mpenzi wake..


Wote walikuwa wamelala chali wanaangalia Gipsum board juu...


" "" " Saidi.. Umeshanijuana hilo ndilo tatizo.. Hupasi kuwa raia tena kwasababu utaiongea hii siri.. 

Unapaswa kuwa kama mimi..

Aliongea Nasra..


" "" " Nakuwa vipi kama wewe jamani.. Kazi zenu ngumu, mnaishi na silaha mda wote mimi nitaweza.??

Aliongea Saidi n kugeuka upande aliolala mpenzi wake..... 


" "" " Si lazima uwe na Silaha.. 

Hii kazi ni akili tu, na si akili ya darasani bali akili ya kucheza na mazingira...

Nimeona Movie uliyo nichezea nikatambua kuwa wewe unaweza sana..

Hata kuwa mbea tu au Shushushu wa kukusanya taarifa unafaa sana..


Hutohitaji nguvu.. Hutohitaji elimu ya darasani.. Bali utaongezewa ujuzi wetu kidogo tu na kazi utaianza.


Tunza Siri ya hii kazi yangu.

 Ukiivujisha ujue umeisha..


ALIONGEA NASRA..


"" "" UUUUUUHHHHH... Saidi alishusha pumzi na kujilaza vizuri huku anatafakari mengi sana akilini mwake..


Muda pia ulikuwa umeenda sana, ilikuwa ni saa 12 na Madakika Jioni..


Nasra aliinuka na kuanza kuanda chakula cha usiku...


"" " Alafu Baby.. Kesho Asubuhi tutoe huu mtungi na haya majiko tupeleke jikoni..

Hii habari ya kupikia chumbani mwisho leo.. Mimi siyo Mpangaji tena, mimi ni Mother House..

Aliongea Nasra na Wote walicheka..


***×***

" "" " Alafu Baby.

 Naweza kukuagiza Mahali.????

Aliendelea kuongea Nasra..


" "" " Wapi tena mpenzi wangu.?? Aliuliza Saidi..

Saidi alikuwa yupo sawa kabisa utadhani siyo yule kichaa aliekuwa anavuruga mashuka na kugaragara chini muda mfupi uliopita...


*******

" "" " Kuna barua yangu ya Bima kanichukulie Pale kwenye Jengo la NSSF.. ukifika wewe Piga honi ufunguliwe geti kisha nenda kaipaki Pikipiki yako sehemu nzuuri na uingie Moja kwa moja hadi Chumba namba 25... 

Ukifika utamkuta mbaba Fulani.. 


Mwambie nimeagizwa na PTIS-041, kisha huyo mzee atakupa kibahasha changu cha bima uniletee.. 


Aliongea Nasra... 


"" "" Poa nipe basi hiyo buku ya bodaboda. Siunajua mimi dereva Boda. Kwahiyo kila napoenda nafunga mahesabu.. 

Aliongea Saidi na kucheka kisha kuinuka... 


"" "" " Saidi.. Hembu vaa suruali ya Jeans na Koti ambalo wenzio hawajalizoea sana ili wasikujue.. Lakini hakuna shida sana muda huu ni usiku hawawezi kukutumbua... 


Wasije wakaanza kukimbia kumuona kichaa anaendesha boda 😂

Aliongea Nasra na wote walicheka... 



Comments