Featured post
- Get link
- X
- Other Apps
ILIPOISHIA.....
Heeeeeehhh We mwanaume wewe.... Nasra alitumbua tu Macho baada ya kuona Hakuna mafuta hata kidogo kwenye Kopo na Saidi alikuwa amejibandika mafuta hadi alikuwa haoni vizuri....
"" "" " Hahahahhah hivi we Saidi umekuwa mtoto eti.. Haya hayo mafuta kujipaka kiasi hicho unamaanisha nini.??
Unanitega eti.. Nitakupiga nikuvunje vunje we niletee ujinga hapa. Hunijui eti we mwanaume..
Aliongea Nasra huku amemkazia Saidi macho kwa hasira sana..
Saidi alishtuka kidogo baada ya kusikia habari za kupigwa. Na vile alishaiona bastola ndio basi tena.. Alijikuta hofu inamtanda na kukimbia bafuni kuoga tena..
Nasra pia aliinuka huku anataka kujua ni wapi Saidi anaenda..
Alinyata hadi mlango wa bafuni na kusikia maji yamefunguliwa...
Saidi alioga huku anacheka cheka mwenyewe..
Baada ya Muda alitoka na kumkuta Nasra kwenye mlango wa bafu..
"" " Dada ulikuwa unatazama mwenendo wa mdogo wako aliekuwa anajimwagia maji ya baraka kuondoa matatizo na nuksi..
Aliongea Saidi na kupita kurudi chumbani..
Nasra alitikisa tu kichwa kuashiria anasikitika, kisha kumfuata Saidi hadi chumbani..
Saidi alianza kukombeleza mafuta kidogo yaliyobaki kwenye kikopo na kujipaka vizuri mwili mzima..
"" " Kumbe akili unazo ila hadi upigwe kwanza..
Aliongea Nasra..
" "" Akili za Geografia na kemia ukijumlisha na Biologia ndio kombi iliyo nifaulisha kwenye shule ya sekondari ya Kata ya Miyuji...
Aliongea Saidi..
Nasra aliinuka na kumenya ndizi kidogo alizokuja nazo na kupika kisha kula na mpenzi wake huku wanatazamana..
Muda wote huo Saidi alikuwa akijichekesha tu kama Mwehu...
Baada ya kula na kushiba walitoka na kwenda sebuleni..
Walianza kuangalia TV chanel ya Mziki lakini baadae Nasra alichukua Rimoti na kubonyeza Kitufe cha (Info) ...
Sehemu ile ilikuwa ikionyesha taarifa mbali mbali.. Nasra aliangalia na kuona Muda fulani Chanel ilibadilishwa na kuwekwa chanel ya Wanyama..
Baada ya Muda fulani Chanel ilibadilishwa tena na kuwekwa ya mziki...
Nasra alitazama muda ule ambao chanel ilibadilishwa kuwekwa wanyama na kutambua ni muda wa asubuhi baada ya yeye kuondoka tu..
kisha alitazama na muda ambao chanel ilirudishwa kwenye mziki na kubaini ulikuwa ni muda yeye amefika nyumbani na kupiga honi..
"" Nasra alikuwa na Akili mingi na muelewa sana.. Alikuwa na uwezo mkubwa wa kutambua mambo haraka hatakama muhusika atakuwa ameficha jambo hilo kwa kiasi gani..
Nasra alikumbuka pia siku ya kwanza anafika kwa saidi.. Alikuta Saidi kaweka chanel ya wanyama. Hadi muda wanafanyiana makabidhiano ya pesa ya chumba hadi kusaini mikataba, chanel iliyokuwa ikionyeshwa ilikuwa ya Wanyama..
Muda wote ambao Nasra alikuwa akifanya mambo yote na kuwaza baadhi ya matukio hayo, Saidi yeye alikuwa anacheza tu kwenye chini kwenye Tiles.
Hakuwa anaelewa chochote kama anachunguzwa...
"" "" Huyu mtoto analeta mchezo na mimi..
Aliwaza Nasra na kumtazama Saidi kwa jicho la kuibia..
******
"" "" Mdogo wangu njoo nikusuke basi jamani...
Aliongea Nasra akimwita Saidi..
""" Unataka unisuke Mithili ya Bob Marley mvuta bangi..
Aliongea Saidi na kumtazama Nasra...
"" "" Yah au hupendi kuwa Rasta man..
Aliongea Nasra...
"" "" Napenda sana. Lakini msuka Rasta ni jangili.. Hawezi kuuona Ufalme wa mbinguni kule Paradiso baada ya Parapanda kulia.. Aliongea Saidi..
"" " Basi sito kusuka..
Njoo nikuchane Nywele zako nzuuuri..
Aliendelea kuongea Nasra na Saidi aliinuka kwenda kukaa kwenye kochi karibu na Nasra....
" "" " Haya.. Njoo lala hapa Mapajani Saidi.
Nasra alizungumza na kumlaza saidi juu ya mapaja yake.
Saidi alilala kwa kutulia kwenye mapaja ya Nasra..
Nasra alichukua kitana na kuanza kumchana Saidi nywele Taratibu huku anampapasa sehemu ya shingo...
Akiwa anaendekea kumchna. NASRA aliongea...
""" "" "" Saidi. Umeona ni Sahihi kunichezea huu mchezo.?? Huoni kama ni upuuzi na unajipotezea muda badala ufanye mambo yako ya msingi..??..
Aliongea Nasra...
Saidi alishtuka kidogo baada ya kusikia Maneno yale na kuanza Kuongea..
"""" Ujue hata mchanga wa Jangwa la Sahara uliwahi vuka bahari baada ya Fimbo ya Musa kukata Mawimbi yaendayo kasi..
Aliongea Saidi akijidai anamjibu Nasra..
" "" " Narudia tena kukwambia Saidi. Mimi si mtoto,
Hadi kufikia sasa nadhani umeshanitambua mimi ni nani..
Najua kuwa ulipekua sana Mabegi yangu wakati sipo na kuanza kusoma vitambulisho vyangu....
Mbaya Zaidi uliishika hadi bastola yangu halafu ukatetemeka ukaiangusha chini..
Saidi Tambua kuwa mimi nilishakusoma Tangu siku ya Kwanza..
Aliongea Nasra na kumfanya Saidi akae kwanza vizuri kwenye Kochi na kuanza kumtazama Mpenzi wake..
ITAENDELEA...

Comments
Post a Comment