Featured post
- Get link
- X
- Other Apps
ILIPOISHIA.....
"" "" " Shkamoo mzee. Nipo nyumbani kwasasa ila nilikuwa nampango wa kurudi kijiweni kuokoteza tena mzee wangu...
Saidi aliongea kwa upole huku anawaza kuna tatizo gani hadi simu ziunganishwe vile....
" "" Sasa kijana. Kuna bwana mmoja anaitwa Sele ni Dalali mkubwa tu hapo mjini..
Leo kaja hapa kwa sababu za kumharibu binti mmoja anaitwa Nasra..
Lakini baada ya mimi kutazama kwa undani nilibaini kuwa huyo Nasra tayari ulishiriki naye kimapenzi..
Aliongea yule mzee...
"" "" Enheee mzee wangu.....
Saidi aliongea na kutulia ili kumsikiliza mzee vyema..
"" "" "" Yule dalali huwa namsaidia kwenye kazi zake nyingi sana hata dawa nyingi za kuoga ili apate mvuto kwenye kazi zake huwa nampa...
Pia huwa anakuja hapa akiwa na Dhumuni la kuwaharibu wake za watu wenye mali ili apendwe na apewe pesa..
Hayo yote huwa namsaidia na huwa anakuja kunipa majibu kuwa mambo yake yanaenda sawa..
Aliendelea kuongea mzee yule
"" "" Sasa leo kaja hapa kwa shida ya kukuharibu..
Daaahh hilo niliona hapana. Niliona haliwezekani kabisa kukufanyia ubaya mtu usiye na Hatia...
Saidi wewe ulimsaidia mwanangu kwa kumpa kazi na kumlipa vizuri bila hiyana yeyote..
Na mimi ndiye nilikutengenezea kinga yako inayokulinda na nilikusafisha hadi ukashinda hiyo bahati nasibu ya mpira na kupata mamilioni yale..
Sasa kwanini nikuharibu kijana wangu pasina sababu yeyote...
Aliendelea kuongea yule mzee..
"" "" " Saidi nakuheshim mwanangu na kama kuna tatizo uwe unanitafuta...
Nimejaribu kumuangalia huyo binti anayo nyota kali ya pesa..
Pia binti huyo nje na kazi yake anayo ifanya, anaonekana kama mpelelezi na huenda anayo kazi ingine ya siri ambayo ni ngumu mtu yeyote kuijua..
Nakuomba mpime huyo binti uone kama anayo mapenzi ya kweli na Umuoe.. Utaona mafanikio yatakavyo kumiminikia..
Alizidi kuongea yule mganga.....
Muda huo Saidi alikuwa kimya akisikiliza kwa umakini sana huku anawaza ni kazi gani ya siri ambayo huenda mpenzi wake anayo..
"" "" "" "
Mwanangu Saidi mimi nakupa moyo wa kuendelea kupiga kazi zako na kujiamini.. Hakuna ubaya wowote. Lakini huyo dalali atakuwa na mwisho mbaya sana aliongea mzee..
Saidi alitulia kimya huku anatafakari nini cha kufanya..
" "" " Basi Mzee wangu. Nimekuelewa.. Mimi leo nikiwa natoka hapa, nitajipatisha ajali ambayo haitoniumiza alafu nitajidai nimekuwa kichaa..
Nataka nipime uvumilivu wa huyu mwanamke. Je ananipenda kweli au kafuata pesa tu.??
Aliongea Saidi..
" "" "" Hilo ni wazo zuri sana.. Hata ukibaini mapungufu yake basi utaniambia tu na mimi nitamtengeneza atatulia sana...
Aliongea yule mzee..
"" "" Dogo Rojas. Kwasasa nitakuwa napatikana kwa sim ndogo tu..
Nitaiweka Silent na nitaificha mbali..
Kama kuna tatizo utakuwa unanitumia ujumbe na nitakujibu ninapo pata muda....
Aliongea Saidia na Mawasiliano yalikatwa na kila mtu aliendelea na Shughuli zake......
*****
Baada ya maongezi yale.. Saidi alishika sim na kumpigia mama yake kumwambia nini anataka kukifanya...
Saidi hakutaka kufanya kwa siri kwasababu aliogopa kumsababishia matatizo mama yake....
Na pia Saidi alikuwa wapekee na msaada mkubwa kwa mama yake.. Aliogopa kumficha mama yake kwasababu mama angesikia kuwa mwanae ni kichaa basi yule mama angepata hata Presha au matatizo mengine ya kiafya...
Saidi aliliamua kumwambia kila kitu mama yake mzazi..
Kwahiyo hata Siku dalali Sele anaenda kwa mama yake Saidi kumwambia habari zile. Yule mama alikuwa anaelewa mchezo wote...
Ni Sele tu ndio alikuwa haelewi nini anakifanya kwasababu kila mmoja alikuwa anamchora tu..
Dalali Sele kwa umbea na akijua anaenda kumkomoa Nasra, alimua kwenda kumwambia mama yake Saidi. Na ndio sababu mama yake Saidi kwenda kumtishia Nasra, Yote ilikuwa ni kumpima tu msimamo wa binti yule..
*******
Huo ulikuwa mpango wote wa Saidi hadi kuwa kichaa...
**********
**********
Siku ya leo baada ya Saidi kujua namna gani maduka yake yanaendelea, aliizima sim na kuirudisha chini kabisa ya begi lake kisha kurudi Sebuleni..
Kabla ya kukaa.. Alipata wazo la kwenda kukagua mabegi ya Nasra..
Aliingia chumbani na kufungua moja ya begi kubwa la Nasra..
Alianza kutoa nguo taratibu hadi chini kabisa ya begi...
Alikutana na mkoba fulani mdogo.. Aliutoa ule mkoba na kuanza kuupekua,
Aliingiza mkono na kushika kitu fulani kigumu cha Plastiki..
Saidi alishtuka na kutoa mkono wake haraka..
Aliingiza tena na kukishika hicho kitu kisha kukitoa...
Alikitazama na kuona ni Bastola...
"" "" Mungua wangu.. Saidi aliongea kwa hofu na kutetemeka sana hadi bastola ikadondoka chini...
"" " Huyu mwanamke ni jambazi jamani... Aliwaza Saidi na kuiokota bastola kuirudisha kwenye Begi..
Alifungua baadhi ya Zipu za kibegi kile na kukuta kitambulisho fulani kidogo kilikaribia kufanana na kitambulisho cha mpiga Kura..
Saidi alikitoa na kukisoma..
" "" " TANZANIA INTELLIGENCE AND SECURITY SERVICE (TISS) ...
Saidi alishtuka baada ya kukuta maandishi hayo na nembo ya taifa pamoja na picha ya Nasra kwenye kitambulisho kile..
" "" " Inamaana huyu Dada ni usalama wa Taifa..??? Aliongea Saidi na haraka alianza kurudisha vitu kwenye Begi kwa hofu...
ITAENDELEA...

Comments
Post a Comment