ILIPOISHIA.....
Nyie mabinti wa mjini mnajidai mnajua kuchezea watoto wa watu kwa kuwaloga ili mmiliki mali zao.. Sasa kwa huyu Mgogo wa Dodoma naomba usahau hilo.. Mali ya mwanangu hakuna mpuuzi wa kuichukua.. Nakupa siku saba mwanagu arudi kwenye hali yake..
Aliongea yule mama na kuinuka kisha kuondoka zake....
Dalali sele aliinuka pia na kuwatazama akina Nasra na Saidi kisha kuondoka zake....
Nasra aliinamisha kichwa huku anawaza na kububujikwa na machozi kama maji..
Alitegemea huenda mama wa Saidi kaja angeweza kusaidiana nae kurejesha hali ya mwanae sawa kumbe ndio matatizo mapya yanaanza..
"" "" " Eeeeehhh Mwenyezi Mungu. Ni mtihani gani umenipa mimi mja wako.. Au kuna sehemu nimekukosea muumba wangu.??? Naomba msamaha wako ewe muweza wa yote....
Aliongea Mwenyewe Nasra na kuchukua kitambaa fulani kwenye kochi na kujifuta machozi pamoja na makamasi yaliyokuwa yanambubujika kwa pamoja...
"" "" Dada Chiku. Huyu mama anatoka wapi,.?? Mbona anawaka kiasi hiki huyu mama.??? Aliongea saidi na kusogea karibu na Nasra kisha kuanza kumbembeleza..
Saidi alikuwa anapenda sana kumuita Nasra kwa jina la Chiku..
Nasra aliingia tena ndani na kunawa uso kisha kupaka mafuta upya na kutoka...
Alimkuta Saidi bado amekaaa tu Sebuleni anaangalia Tv huku anacheka...
"" "" Saidi. Naomba ukae hapa nyumbani kwa kutulia.. Kama hupendi niendelee kuteseka na kulia, basi nakuomba sana usitoke humu ndani..
"" " Mimi natoka sasaivi kwenda kazini. Nakuomba basi njoo ufunge Geti na urudi ndani utulie Saidi.. Nakuomba sana...
" "" " Sawa dada Chiku.. Nakutakia kila Kheri mbele ya mboni ya macho yako.. Usifikirie mengi sana juu ya nyota inayong'aa upande wa kusini mwa Dunia..
Angalia nyota ya Magharibi ndio inayomulika ulimwengu kwa uangavu wa hali ya juu..
Haya unaweza kwenda..
Aliongea Saidi na kuinuka kisha kumshika Nasra Mkono na kuelekea nae hadi lilipo gari..
Nasra alipanda na alifunguliwa vyema tu gati na Saidi kisha gari likatoka..
Saidi alirudishia geti na kurudi Sebuleni..
Saidi alishusha pumzi na kutulia kimya utadhani hana matatizo ya akili, aliwasha TV na kuanza kuangalia baadhi ya vipindi...
Alishika rimoti na kuweka chaneli ya wanyama kwasababu alikuwa mpenzi sana wa kuangalia mambo hayo...
Saidi aliinuka tena na kwenda kufunga vizuri mlango wa Sebuleni na kuingia chumbani kwake..
Alifungua begi lake na kuangalia hati zake za nyumba....
Aliziona zote zipo sawa..
Aliendelea pekua zaidi ndani ya begi na kuchukua simu yake ndogo iliyokuwa silent kisha kumpigia mmoja wa wafanyakazi kwenye duka lake la Jumla..
"" "" Rojas, mambo vipi mzee, aliongea Saidi na kuiweka ile simu Laud speaker..
"" " Poa brother.. Unaendeleaje.. Alijibu huyo Rojas
""" mimi nipo poa kabisa.. Nimepata nafasi ndogo hapa nikaona nikucheki..
Vipi pesa za mapato yote unaingiza kwenye account.??
Hakikisha na wafanyakazi unawalipa kwa wakati.. Kama kuna tatizo nitumie tu ujumbe. Kama sintokujibu kwa wakati basi ujue nipo bize.. Lakini nikiwa Free nitakuwa nakupigia...
Aliongea Saidi huku anachungulia Dirishani kama kuna mtu anatokea au laa...
"" " Sawa Broo...
Usijali kila kitu kipo sawa. Nakutakia kila la kheri katika kumpata mke mwema..
Aliongea Rojaz na kukata sim...
*******
Kumbe saidi hakuwa na Tatizo lolote la Akili lakini ukweli ni kwamba Dalali sele alikuwa na mpango wa kumharibu mwenzie na inasemekana kuwa ni tabia yake hapo mtaani..
******
Siku ya Tukio iliyo pelekea Saidi kujipatisha ile ajali Makusudi ilikuwa hiviiiiiiii
****
**
Mara tu baada ya Dalali sele kutoka Ndachi kwa mganga na kufanya mambo yake kama alivyohitaji yawe.....
Yule mganga alishika simu yake na kumpigia mwanae Rojas, kumbe Rojas yule mfanyakazi na msimamizi wa maduka ya Saidi alikuwa ni mtoto wa yule Mganga lakini Dalali sele hakuwa anajua kitu chochote...
"" "" Mwanangu Rojas, nakuomba sana mjulishe Boss wako kuwa kuna kijana fulani kaja hapa kwa nia ya kutaka kumfanyia dawa awe kichaa kisa ugomvi wa mwanamke...
Huyo jamaa nilimsikiliza tu na kumwambia kuwa nitamfanya Saidi kuwa kichaa..
Amelipa pesa yule jamaa na mimi nilifanya kazi ya uongo tu hapa...
Aliongea yule Mzee..
"" "" " Hembu ngoja baba... Nampigia Saidi ili asikie yote haya..
Aliongea Rojaz na kumpigia Saidi pia..
Ziliunganishwa simu tatu na walikuwa wakisikilizana Vyema tu...
" "" Mwanangu Saidi upo wapi.. Aliongea mzee baada ya Saidi kupokea simu na kujiunga na Mjadala huo.....
"" "" " Shkamoo mzee. Nipo nyumbani kwasasa ila nilikuwa nampango wa kurudi kijiweni kuokoteza tena mzee wangu...
Saidi aliongea kwa upole huku anawaza kuna tatizo gani hadi simu ziunganishwe vile....
ITAENDELEA...
Comments
Post a Comment