MUHOGO NDANI YA GEREZA 09


 



"ni nini hiki?" askari huyo aitwae afande Rukia alituuliza huku akitazama urenda urenda kwenye vidole vyake, nikagundua ni wazungu waliotoka kwenye dudu langu wakati nilipolichomoa kutoka kwenye uchπŸ€” wa mwanadada Queen, kumbe waliruka umbali mrefu namna hiyo, mita kadhaa kutoka kitandani tulipokuwa tukipeana raha mimi na Queen


"mh hatujui afande!" nilijibu afande huyo akatutazama tu

"rudi shambani!" aliniamrisha mimi nikatoka taratibu na kwenda shambani nikimwacha Queen peke yake na askari huyo wa kike 


 Nilipofika shambani nikakuta wenzangu waliokuwa wanaendelea kulima wakiwa wamefika mbali sana, nikajiunga nao nikianza kulima kipande changu kilichokuwa kipo vilevile nyuma nyuma wala hakijaguswa kabisa ikabidi nianze mwanzo mpaka niwafikie wenzangu waliotangulia 


 Mwanaume atabaki kuwa mwanaume tu, nililima kwa nguvu zangu zote mpaka nikawafikia walipokuwa wenzangu huku afande Rukia nae akija kuungana na askari wenzake kutusimamia akiwa amemwacha Queen peke yake ambae alikuwa wala haumwi chochote ikiwa ni gia tu ya kutafuta nafasi ya kupata faragha na mimi akiwa amefanikiwa kukipata alichokitaka lakini siyo kwa namna aliyoizoea yeye ya kugusana gusana na yule mwanamke mwenzake ila kwa namna yenyewe halisia kabisa, ya 'kupigwa rungu' lile lenyewe halisi kabisa kabisa, muda wote Anitha akinitazama tu pembeni huku akiendelea kulima, afande Rukia akawa nae akinitazama kwa makini muda wote nilipokuwa ninalima na wenzangu, nadhani alihisi kuna kitu kisicho cha kawaida kinaendelea kwangu maana alikuwa akinitazama muda wote


 Tulimaliza kulima saa moja kila mtu akawa anakunywa maji wengine wamejilaza chini, ingawa tulikuwa wengi lakini kiufupi kazi ilikuwa nzito siku hiyo 


 Ilipofika majira ya saa tatu kwenda saa nne hivi asubuhi afande Rukia alinifuata na kuniita, nikamwitikia na kumfuata askari huyu ambae nilihisi kama ameanza kunitilia mashaka


"abee afande!" nilimwitikia nikiiweka vizuri hijabu yangu huku nikitabasamu 

"asallam aleykhum!"  alinisalimia nikabaki nikicheka cheka kumzuga

"jamani afande wewe una utani mwingi, walleykhum salaam"

"hebu vua hijabu yako hiyo!"

"abee afande??"

"nimesema vua hijabu yako!" afande Rukia alikuwa mkali 

"lakini afande si sheria ina...... "

"unabishana na mimi askari?" afande Rukia alikishika kirungu chake akitaka kunitandika nacho


"wewe Reshma unahitajika getini!" kwa bahati nzuri afande Jane akatokea na kuniita akaniepusha bila kutegemea kutoka mikononi mwa afande Rukia nikamwitikia afande huyo na kumfuata nyuma nyuma


Nilipofika nikakutana na mwanasheria wangu au wakili kwa jina jingine akiwa amekaa ananisubiri na suti na tai yake na mafaili kadhaa, nikakaa kwenye kiti kumsikiliza wakili wangu huyo ambae hata yeye hajui kama mimi ni mwanaume kama yeye 


"unaendeleaje?" aliniuliza

"salama habari?" niliongea kwa sauti yangu ya kike kama kawaida yangu mpaka kesi hiyo itakapoisha ndipo nitabadili muonekano wangu na kujirudisha katika uwanaume wangu nisije nikatungiwa kesi nyingine nikaongeza matatizo na nikaharibu ushahidi


"nimekuja kuna jambo nataka kukushirikisha kidogo uniwie radhi" wakili huyo aliniambia akijiweka sawa nikahisi lazima kuna kitu kitakuwa hakipo sawa maana siyo kwa kauli hiyo ya 'niwie radhi' 


"Naam nieleze tu wakili wangu!"

"nasikitika kukuambia kwamba sitaendelea na kesi yako hii tena bi Sherma ninabwaga manyanga unaweza ukamtafuta wakili mwingine wa kukufaa" wakili aliniambia nikashusha pumzi ndefu sana huku nikijiinamia na kutazama chini kwa masikitiko maana kesi yangu yenyewe bado wiki mbili tu isikilizwe tena


"sawa asante ndugu wakili usijali asante hata kwa hapa uliponisaidia Mungu akubariki sana na ninakutakia majukumu mema!"

"sawa mimi naenda bi Sherma" wakili alinipa mkono nami nikaupokea


"asante sana wakili, safari njema!" nilimjibu tukipeana mkono na wakili huyo ambae alinitekenya kwenye kiganja cha mkono huku akitabasamu nikabaki nikimshangaa wakili huyo nikiwa simuelewi elewi, akabeba begi lake na kuondoka nami nikarejea ndani kwa wafungwa wenzangu nikiwa nimenyong'onyea kweli


"kulikoni Paul?" Anitha aliniuliza aliponiona nimenyong'onyea nimejiinamia chini

"mh kawaida tu!"

"nishirikishe basi Paul mume wangu kuna shida gani mbona kama haupo sawa!"

"wakili wangu ameghairi kusimamia kesi yangu!" nilimjibu nikiongea sauti yangu ya kawaida ya kiume 


"ni kweli ninachokisikia au uwongo?" mara tukamsikia mtu nyuma akituuliza tulipogeuka kutazama tukakuta ni afande Rukia kumbe alikuwa nyuma akitusikiliza maongezi yetu


"afande???!!!" tulishtuka baada ya kumuona...... 


Inaendelea



Comments