MUHOGO NDANI YA GEREZA 05

 




 Kikombe changu cha chai kilipigwa ngumi nzito kikaruka juu juu na kujigeuza geuza huku chai ikimwagika juu kwa juu karibia inimwagikie chai hiyo ya moto na kikombe kikarudi chini sakafuni kikidundadunda kama kitenesi


 Nikabaki nikimtazama mwanamke huyo 'jike dume' ambae alibaki akiwa amenikazia macho kwa hasira, huku 'mwanamke' wake akiwa ametulia tuli akiogopa 


"mlikuwa mnafanya nini?" aliuliza

"nilikuwa nampunguzia chai tu mbona unanimwagia chai yangu tatizo liko wapi?"

"unampunguzia chai demu wangu kwa ruhusa ya nani?" mwanaume huyo aliniuliza kwa amri kana kwamba yeye ni mwanaume kumbe ni mwanamke tu kama wengine sema akiwa na vijitabia na hulka za kiume


"sasa mbona unafika mbali kumpunguzia chai kuna tatizo wakati ni jambo la kawaida tu!"

"halafu wewe demu mgeni usiniletee dharau umesikia wewe utapaona jela pagumu!" mwanadada huyo mnene mnene kidogo mwenye kifua na mfupi kiasi alinijibu akinikunja na kunikwida nguo yangu akijua mimi ni mwanamke mwenzake, askari walikuwepo lakini wakitazama tu kinachoendelea bila kufanya lolote, wafungwa wengine wakaanza kushangilia kwa kupiga makofi na kutuchochea tupigane


"niachie tafadhali!" nilimwambia nikiutoa mkono wake, 

"Censia muachie mwenzako kwani amekukosea nini?" Anitha rafiki yangu nae alijaribu kunitetea mbele ya mwanamke huyo ambae jina lake halisi kwa nilivyosikia ni Mwajuma lakini wakimbatiza jina la mwigizaji nguli wa kike 'Cynthia' na mpiganaji nguli, kutokana na tabia zake za ukorofi na kupenda kupigana pigana


 Alimsukuma Anitha ambae kutokana na kukosa pa kujishikiza alainguka mpaka chini mzima mzima jambo ambalo sikulifurahia nikautoa mkono wa mwanadada huyo 'Cynthia' na kuutupa kwa nguvu, akakasirika na kurusha ngumi ambayo nilikosea kuiotea ikatua shavuni mwangu ikiniingia kisawa sawa, ingawa ilikuwa ya mtoto wa kike lakini mikono yake ilikuwa imekomaa akionekana ni mfanya mazoezi ya mwili 


 Censia alirusha ngumi nyingine ambayo alidhani ataniotea tena lakini niliiyona na kuudaka mkono wake kisha nikamrushia ngumi nzito ya uso ambayo niliizuia kwa kumuhurumia ikaishia usoni mwake ikimgusa tu puani, laiti ingemshukia nadhani asingesalimika, nilikumbuka kuwa ni mtoto wa kike tu atabaki kuwa hivyo, sina haja ya kupigana nae


"piga huyo Sherma mpigee!" Anitha alinihamasisha akiwa na kisasi baada ya kuangushwa pale chini


"siyo kila umwonae ndiye ndivyo ilivyo mwingine siye!" nilimwambia mwanadada huyo kwa fumbo ambalo hakulielewa, nikarudisha ngumi yangu ambayo haikumfikia na kumletea madhara yoyote na nikamwachia mkono wake 


"kuna nini kinachoendelea hapo eeh!" afande Rukia akajifanya kusogea baada ya kuona pambano limehairishwa kila mfungwa aliyekuja kuona ugomvi huo akarudi kwenye meza yake, pamoja na mimi na Anitha na yule dada mwingine niliyetaka kumpunguzia chai, tukakaa kwenye meza moja huku 'mwanaume' wake bado akiwa anaendelea kututazama kwa hasira, hasa mimi, akiwa kwenye meza yake aliyokaa


"samahanini kwa yaliyotokea!" yule dada aliyeniomba chai ambae mtu wake ametuletea fujo alituambia mimi na Anitha


"mssssyuuu!" Anitha akasonya

"usijali chukua muhogo huu!" nilimjibu kwa sauti ya kike kama kawaida yangu nikimpa kipande cha muhogo ambacho alikipokea kwa mashaka huku akimtazama mtu wake yule Censia ambae aliendelea kumtisha tisha


Muda wa chai uliisha sasa ikawa ni kila mtu kwenye usafi, mwenye nguo akafue nguo zake, mwenye kusafisha chumba chake asafishe na kila aina ya usafi, mimi nikatumia muda huo ambao kila mtu alikuwa bize kwenda kuoga bafuni kimya kimya, tena nikaoga haraka haraka kabla sijakutwa kisha nikarejea chumbani nilipomkuta Anitha akifagia fagia huku yule mwanadada mwingine ambae anaitwa Queen akiwa amekaa kitandani kwake akinitazama tu, yule ambae nilimpunguzia chai, mchumba wa Censia


"ulikuwa wapi Sherma!" Anitha aliniuliza

"nilikuwa huko nje natengeneza tengeneza viatu vyangu!"

"nje wapi mbona una maji kichwani?" Anitha alinishtukia

"nimenawa tu kichwa!"

"umenawa au umeoga wewe wakati mwili wa baridi kabisa hebu toa ushungi wako huo!" aliniambia akitaka kunivua

"uache bwana!" nilimjibu nikimzuia 


"mwache tu anapendeza sana akivaa hijabu yake!" Queen aliyekuwa kitanda cha pili aliongea 

"kelele nawewe maongezi yetu yanakuhusu nini?" Anitha alimjibu kwa hasira huku akinifuta futa maji na wakati huohuo kumbe yule Censia alikuwa mlangoni amesimama akiona kinachoendelea, akamfuata mpenzi wake huyo kitandani


"umeanza kupenda penda mtu mwingine eeh mpaka unamsifia kuwa anapendeza bila hata aibu?" 


"hapana nimesema tu hijabu yake imempendeza siyo kama ninampe.. " kabla Queen hajamaliza sentensi yake hiyo alichapwa kofi la shavuni na Censia


"nyamazaaa mjinga mmoja wewe!" Censia alimkaripia mwanadada huyo akitaka kumtwanga ngumi lakini nikamuwahi na kumdaka mkono wake


"mwache!" nilimwambia,

"achilia mkono wangu!" alinijibu nikwamwachilia akatoka ndani ya chumba hicho kwa hasira, Anitha akawa amesimama kwa pembeni akionekana kuchukizwa na kitendo cha mimi kumtetea tetea Queen


 Siku hiyo ya mapumziko iliisha na hatimae usiku uliingia baada ya kula jioni tukapanda vitandani saa tano za usiku kwa amri na askari wakitembea kwenye korido kuhakikisha kila mmoja amelala, mimi nikiwa nimelala na Anitha ambae hakuniongelesha chochote akionekana kukasirishwa na mimi hasa kitendo changu cha kumtetea tetea Queen kutokana na matendo anayotendewa na Censia


"Anitha umelala dia?" nilimwuliza nikimgusa begani akiwa amegeukia upande wa pili

"bwana usinisumbue Sherma!" alinijibu akiutoa mkono wangu nisimguse

"yamekuwa hayo jamani nisikilize basi" nilimjibu nikimshika kiunoni, Anitha akashtuka kidogo na kutulia kwa sekunde kadhaa mkono wangu ulipokuwa kiunoni mwake kisha akageuka na kunitazama, nikatoa mkono wangu lakini akaurudisha tena kiunoni mwake


"nikueleze au nikuonyeshe nini Sherma ujue kama nakupenda naumia unapoanza kumjali mtu mwingine!" Anitha aliniambia


"mh Anitha mimi si.....!" kabla sijazungumza Anitha akinisogezea midomo yake kinywani mwangu na kuanza kuninyonya mate taratibu.......


Inaendelea..

Comments