Nilibaki nikipepesa pepesa macho nikiwa siamini amini kama ndiyo kweli naingia gerezani kwa mara ya kwanza
"tembea wewe!" askari mmoja wa kike aliyekuwa nyuma yangu alinisukuma kumbe nilikuwa nimejisahau nikasimama bila kujua nikawa nimeduwaa baada ya kusukumwa ndipo nikashtuka kutoka kwenye bumbuwazi,
Tulifika mpaka sehemu ya mapokezi kwa askari mmoja ambae alipewa karatasi ya majina yetu, akatutazama na kutukagua kagua kisha tukapelekwa mpaka chumba maalumu cha kubadilisha mavazi, tuyatoe yale tuliyokuja nayo ya kiraia ili tuvae sare za kimahabusu tufanane na wengine, mtihani ukawa upo hapo, tuliingizwa wote saba kama tulivyo, tukaanza kubadilisha nguo, askari huyo wa kike akiwa nje anatusubiria
Wanawake hao wafungwa mahabusu wenzangu walianza kuvua nguo zao mbele yangu wakijua mimi ni mwanamke mwenzao nikabaki nimeganda nimesimama natazama pembeni nikikwepa kuwatazama maana mambo lazima yabadilike kama mwanaume unapomwona mwanamke akiwa mtupu (uch🤔) na nikagundulika bure kama siyo mwanamke, ni mwanaume kamili tena rijali
Wakati nikiwa nimegeukia pembeni nisiwatazame wanawake hao mmoja alikuja huku huku mbele yangu akisimama akiwa uch🤔 hana nguo
"ohooo huyu nae vipi?" nilijisemea kimoyomoyo nikageuza kutazama upande wa pili kumkwepa nikakutana na wale wengine bado baadhi nao wakiwa uch🤔 wengine wakiwa wamevaa tayari sasa nikawa nimefanya 'ushubwada' kama vijana wa sasa waitavyo, nakwepa kumtazama mmoja najikuta nawatazama wengine wanne, ikabidi nigeukie kwa huyu huyu aliyekuwa peke yake huku ndo dah! nilijikuta kwenye wakati mgumu maana alikuwa ameinama yaani amebong'oa akihangaika kuvaa suruali ya sare ya mahabusu makalio yake ameyaelekezea kwangu akiwa amevaa chup🤔 tu, Jogoo wangu akasimama dede ndani ya baibui nililovaa lakini kwa sababu lilikuwa pana pana nikanusurika kujulikana
"mbona huvai shosti umeganda tu hapo?" aliniuliza
"ndo navua hapa namimi ngoja nije nikusaidie naona unapata tabu" nilijibu huku nikizuga kulishusha baibui langu lakini nikivua kwa mahesabu nisije kujulikana kama siyo mwanamke mwenzao
"njoo unisaidie tu utakuwa umefanya la maana shosti maana hii nguo mh changamoto"
"sawa!" nilimwitikia nikibana sauti yangu kama ya kike na uzuri kipaji hicho nilikuwa nacho tangu shuleni cha kuiga sauti za watu maarufu na mpaka wanawake, mpaka nilipata kesi siku moja nilipokuwa sekondari kidato cha tatu, nilipowatangazia wanafunzi wenzangu darasani kwetu kuwa kuna kikao cha wazazi nikiiga sauti ya mwalimu mkuu wa kike huku nikiwa nimejibanza wasinione na nikawaruhusu waondoke shuleni kama utani lakini kwakuwa hawakuniona nilijibanza na sauti ya mwalimu mkuu naipatia haswa wakaniamini na kuondoka shuleni kabla ya kengele ya mwisho ya kutoka madarasani kupigwa
Jambo hilo lilinifanya nipewe adhabu ambayo sikuwahi kuipata, nitandikwe bakora zisizo na idadi, tena siyo kwa mwalimu mmoja ila wote shule nzima, adhabu ambayo sitokaa niisahau kamwe, yaani maisha yangu yote
Nilimsogelea yule mfungwa wa kike mahabusu mwenzangu aliyekuwa akihangaika kuvaa suruali yake ya sare bila mafanikio nikachuchumaa akiwa na chup🤔 tu tena kifuani akiwa wazi matiti yake yananing'inia nikaanza kumsaidia kumvalisha, mimi nikiwa hata bado sijaanza kuvaa zangu
"uuuwiii!" alishtuka nilipomshika mguu akihisi kama ameguswa na kitu cha tofauti, nadhani alihisi kama kutekenywa hivi sababu ya jinsia yangu kwa hiyo ile kanuni ya 'hasi na chanya ilifanya kazi yake, au ile ya sumaku na chuma' kuvutana
"kulikoni mbona tunashtuana?" mmoja aliuliza, wote waliokuwa pembeni wakitushangaa
"hamna kanigusa tu kwenye kidonda mguuni niliumia!" yule mwanadada alizuga
"pole na samahani kama nimekuumiza!" nilimwambia kama kawaida kwa sauti yangu ya kike
"asante usijali!" aliniambia huku akitabasamu na kunitazama usoni, machoni kwa sekunde kadhaa akinikazia macho yake
"hey hey hamjamaliza tu mnadhani mpo majumbani mwenu mnajipodoa?" yule askari aliyetuleta aliongea kwa ukali akiupiga mlango kwa nguvu na kutushtua mle ndani kila mtu akaanza kuhangaika haraka haraka kumalizia kuvaa, kazi ikiwa kwangu kulivua juba langu, haraka haraka nikaanza kulivua wote wslipokuwa wakihangaika kuvaa nami nikiwa nimegeukia ukutani lakini yule niliyemsaidia kuvaa suruali yake ya sare alikuwa bado akinitazama, nadhani hakuwa na uhakika namimi,
Wote walikuwa wameshamaliza kuvaa wakitoka ndani ya chumba hicho haraka haraka nikabaki mimi tu peke yangu nikihangaika kuvaa na ndipo yule askari akaingia na mwenzake wakiwa na virungu vyao mikononi, wote wakiwa askari magereza wa kike kutokana na kuwa ni gereza la wanawake, wakiwa na kofia zao vichwani
"halow kwahiyo wewe ndo husikii amri?" askari yule mwingine aliniuliza huku akigonga gonga kirungu chake kwenye mkono wake akimaanisha hakuna usalama kwangu, wote wawili wakinifuata
"hapana afande nguo tu ilikuwa inanisumbua halafu nilikuwa namsaidia yule paa.... le mwenza......ngu!" nilijitetea kwa sauti ya kike kama kawaida yangu huku nikirudi kinyume nyume kwa wasiwasi
"hapana afande nini nini na nini, unaongea kama upo chumbani na mumeo... tumfanyaje huyu afande?" askari mwenzake alinijibu kwa kubana sauti akiiiga sauti yangu iliyoonekana kama ya mapozi sana huku akimwuliza afande yule mwingine
"huyu ni wa kutandikwa mpaka ajinyee, aelewe hapa siyo kwa mumewe, ni gerezani"......
ITAENDELEA
Comments
Post a Comment